- Eti babu wa Loliondo anafunguliwa kesi za jinai na madai. Anafunguliwa kesi ya jinai kwa kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kwamba eti aliwahadaa watu kwamba dawa yake inatibu wakati hakuna mtumiaji aliyepona.
- Pia anafunguliwa kesi ya madai ili aweze kulipa fidia za watu waliopoteza maisha na wote waliosafiri kutoka sehemu mbalimbali huku wakitumia gharama kubwa ili kupata dawa isiyotibu.
Lakini je:
- Vipi kuhusu mawaziri na vigogo wa serikali waliokuwa wakimiminika Loliondo huku wakiifagilia dawa hiyo kwamba ilikuwa imewasaidia na hivyo kuendelea kuchochea moto wa tiba hiyo? Hawahusiki kwa namna yo yote na "utapeli" huu?
- Vipi kuhusu ripoti ya "wataalamu" iliyosema kwamba kikombe cha babu kilikuwa ni tiba bomba? Vipi kuhusu wagonjwa waliokuwa wakisimama na kuitetea dawa hiyo kwamba ilikuwa inatibu? Vipi kuhusu watoa vikombe wengine waliokuwa wamechipuka sehemu mbalimbali nchini? Nao watashtakiwa?
- Maswali ya kujiuliza katika suala hili ni mengi na yote yanaonyesha jinsi tunavyoendesha mambo yetu kama jamii. Hatuko makini, hakuna uwajibikaji na mambo yetu mengi - hata yale ya muhimu kabisa - tunayafanya kimzahamzaha tu. Kama anavyosema mhusika mmoja katika vibonzo vya Pogo, adui wa maendeleo yetu si mwingine bali ni sisi wenyewe!
- Jikumbushe habari mbalimbali kuhusu Babu wa Loliondo na "tiba" yake ya kimiujiza HAPA.