Adverts

Jan 22, 2012

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi,(CCM) Nape Nnauye Ashiriki Kwenye Mahafali Ya Shule Aliyosoma Mkoani Mwanza

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akikaribishwa na Mkuu wa shule ya sekondari Nsumbi, Mwanza juzi alipowasili akiwa mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha sita ya shule hiyo.
Nape akiwa na viongozi wa shule wakiwa wamsimama kuwakumbuka wanafunzi wawili wa kidati cha sita waliofariki dunia hivi karibuni.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimkabidhi cheti mhitimu wa kidato cha sita, Burilo Busagi, katika mahafali ya kidato cha sita shule ya Sekondari Nsumba, Mwanza. Jumla ya wahitimu 374 wa kidato hicho walipewa vyeti. Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo Josephat Zakeyo
Nape akiwasalimia wahitimu wa kidato cha sita waliokuwa wakimsubiri awatunuku vyeti katika mahafali ya shule ya sekondari ya Nsumbi, Mwanza. Kulia ni Mkuu wa shule hiyo, Jozephat Zakeo.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape NNauye akikagua moja ya mabweni ya shule hiyo kabla ya kutunuku vyeti kwa wahitimu wa kidato cha sita shule ya sekondari Nsumbi, Mwanza juzi. Bweni hilo analokagua ndilo alitumia aliposoma kidato cha nne katika shule hiyo mwana 1994 hadi 97. Wapili kushoto ni Mkuu wa shule hiyo Josephat Zakeo.
Nape akikagua ujenzi wa jengo jipya katika shule hiyo.
Nape akikagua leo bweni alimokuwa akilala wakati anasoma kidato cha nne katika shule ya Nsumbi, Mwanza mwaka 1997.
Wahitimu wakishangilia hotuba ya Nape.
Wahitimu wa kidato cha sita wakiingia kwa wimbo maalum kwenye ukumbi wa sherehe za mahafali yao.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na mwanafunzi aliyesoma shule ya sekondari ya Nsumba, Mwanza, kati ya mwaka 1954 na 1957 (darasa la nane na kumi) Damas Ngoma, wakati wa mahafali ya kidato cha sita ya shule hiyo juzi. Nape ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo alisoma pia katika shule hiyo hadi kidato cha nne ambacho alimaliza mwaka 97. Watatu ni Mkuu wa shule hiyo Josephat Zakeo.