Jan 7, 2012
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUFUNGULIWA KESI
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUFUNGULIWA KESI: MWANASHERIA wa kujitegemea wa jinini Mwanza Stephen Magaigwa amekusudia kufikisha hati yake ya mashitaka kuwafungulia kesi Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Mahakama kuu Maalum ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na wanasheria hao kuruhusu makosa muhimu manne yanayokinzana yaliyomo katika katiba ya Jamhuri na ile ya Mapinduzi.Mwanasheria Stephen Magaigwa.
Amesema kuwa Kupitia marekebisho ya katiba ya mwaka 1977 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Zanzibar ya mwaka 1984 tangu nchi hizi mbili zilipoungana kuna mambo walikubaliana kwamba haya ni ya Muungano lakini yamekiukwa kupitia marekebisho yaliyofanywa ya katiba ya Zanzibar.
"Baada ya kutumia taaluma yangu kifungu baada ya kifungu nimegundua kuwa marekebisho hayo yameingilia mambo ya Muungano na kuleta mkinzano au mkanganyiko katika shughuli za kila siku za utendaji wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania".
"Nilitegemea kuwa wanasheria wa serikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wangechukuwa hatuwa maalum kurekebisha hali hii tangu awali kabla ya kuipeleka katika utekelezaji lakini walikaa kimya kama wataalamu wa sheria wasiojuwa kazi yao.
Mambo manne aliyogundua" Mbele ya wandishi wa habari.
1.Haki za binadamu:- "Katika marekebisho ya katiba ya Zanzibar suala la Haki za Binadamu katiba hiyo imezua kwamba haliwezi kuja katika Mahakama ya Rufaa –Wakati Ukisoma katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jedwali la 1 unagundua kuwa suala la Mahakama ya Rufaa ni suala la Muungano"
"Lakini Haitoshi linapokuja suala la haki za binadamu nchi inayohusika ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"2.Ukisoma Marekebisho ya Katiba ya Zanzibar kifungu cha 2A Rais wa Zanzibar anaweza akaigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo mengine kadri atakavyojisikia – Lakini kifungu cha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2(2) Suala la Mipaka ya nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni suala la Muungano hivyo Rais akitaka kuigawa sehemu ya Jamhuri ya Muungano (Tz bara na Tz visiwani) ni lazima awasiliane na Rais wa Zanzibar Lakini ya Zanzibar inasema anaweza kugawa bila kuwasiliana na Rais wa Tanzania, sasa tuna nchi moja ambayo imeungana kwenye mipaka lakini watu wawili wanaohusika kuigawa.
3.Majeshi ya Ulinzi:- "Katiba ya Jamhuri inasema kuwa nchi pekee ambayo imepewa mamlaka ya kuunda majeshi ya ulinzi au vikosi vya aina yeyote ile ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lakini Marekebisho ya kumi ya sheria namba 9 ya mwaka 2010 ya katiba ya Zanzibar yanasema sasa wanaweza kuunda vikosi kama KMKM na kadhalika … Swali ni nani Amri Jeshi Mkuu wa majeshi hayo? Kwani yanapoundwa lazima yawe na mtoa amri wake mkuu"Katiba zinazokinzana.
4.Wakuu wa nchi wawili:- "Ukisoma katiba ya Zanzibar 26(1) na ile ya Muungano kifungu cha 33(2) utagundua kuwa sasa tuna wakuu wa nchi wawili, sasa tunapokuwa na wakuu wawili ile hali katika katiba hatua ruksa ya kuwa na ‘two head of state in one country’ hali hii inamaanisha nini?" "Nimefungua kesi hii Mwanza kwa mujibu wa Kifungu cha katiba ya Jamhuri 126-127 na 128, hivyo shauri langu litakapo sajiliwa na kupatiwa hati ya Mashitaka, Rais atapewa taarifa kuteuwa majaji wa kusikiliza kesi hii maalum ya katiba kwenye mahakama maalum ya katiba"
Lengo kuu:- Nitaomba Mahakama hiyo iamuru katiba ya Zanzibar irekebishwe kuondoa kasoro hizo haraka iwezekanavyo ili kuleta sifa ya Muungano.