Adverts

Jan 9, 2012

MWENYE KIJIKO HAYAWEE, MWENYE KIKOMBE HAYAA, GUDURIA HAYA!!!!

Picture
Na Francis Godwin, Iringa
Wakazi wa Tanangozi na Ihemi katika wilaya ya Iringa vijijini katika harakati za kukinga mafuta kutoka kwenye lori la kusafirisha mafuta lenye namba T 575 AXH lililoanguka na kumwaga mafuta katika barabara kuu ya Iringa-Mbeya eneo la Ihemi, huku polisi wakishuhudia bila kuchukua hatua zozote endapo mlipuko utatokea.
Ni jambo la kushangaza sana kuwa baada ya visa vya watu kulipukiwa na moto wa mafuta ya dizeli au petroli si tu nchini mwetu bali hata nchi jirani kama vile Kenya, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Nigeria nk, licha ya habari na taarifa hizo za kutisha ambazo zimeua maelfu ya watu, watu bado wanasogelea hatari hiyo.
Ni kama vile tahadhari zinazotolewa za kutokukaribia hatari hiyo zinapuuzwa, au watu wana kiburi kwa kujiamini wao ni spesheli na wajuzi zaidi kamwe hawawezi kukumbwa na hatari au ni ujinga ama kutokujali na kusingizia maisha magumu.
Kama hiyo haitoshi, wanaonekana baadhi ya askari nao ambao jukumu lao la msingi ni kulinda usalama wa raia katika hali yoyote, anaonekana kukubaliana na kinachotendeka mbele ya macho yake. Nilitarajia wawe mstari wa mbele kuweka utepe wa njano kuzunguka eneo lenye lori hilo na kuhakikisha yeyote anavuka utepe huo anatiwa nguvuni na kufikishwa mahakamani kwa kuhataria maisha yake, ya jamii na kukiuka maelekezo halali ya askari.
Kweli, "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa!" - Hosea 4:6
Picture
Askari ni kama vile nao ni... kwa jinsi alivyosimama na kuonekana kuacha anachokishuhudia kiendelee kana kwamba hakumbuki kazi yake ni kulinda usalama wa raia nyakati zote.
Picture
Na watoto wamo katika hatari hiyo pasina kutaka. Picha na Francis Godwin