Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo (kushoto) akitoa tamko jana jijini Dar es salaam kuhusu hatma ya wanafunzi waliofutiwa matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2011 ambapo Serikali imeamua watahiniwa 9,629 waliofutiwa matokeo kutokana na kubainika majibu yao kufanana kurudia mtihani wa darasa la Saba mwezi Septemba mwaka huu 2012 Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Elimu ya Msingi Zuberi Samataba.Picha na Vicent Tiganya-MAELEZO