Adverts

Jan 6, 2012

Ni Kusanyiko La Magezi-gezi? Wakufunzi Wa Wakufunzi!

Ndugu zangu, Moyo wangu ulidunda, mara ile nilipopokea na kusoma mwaliko wa kujumuika na kusanyiko la wanahabari waliobobea na wenye majina makubwa. Ni kwenye mafunzo ya wakufunzi wa wanahabari. Kaka yangu Kajubi Mukajanga anasema; Wahaya wanamwita mtu anayejifanya anayejua jua sana mambo kwa jina la ' Lugezi-gezi'- Kwamba yeye anajua kila kitu!" Nami nilidhani ningefika Morogoro na kukutana na watu wenye hulka ya 'lugezi-gezi'- wajuaji wa kila kitu. Kwamba nisingekuwa na kipya cha kuwaambia. HAPANA! Kusanyiko hili la Morogoro limeniondoa mashaka hayo. Kila mmoja anaonekana kuwa na utayari wa kujifunza kutoka kwa mwenziye. Kuna utani mwingi pia. Tunacheka sana. Tunajifunza. kutoka mjengwa blog Naam, kusanyiko la Morogoro lina waandishi wenye uzoefu wa miaka mingi kwenye tasnia ya habari. Kuna majina kama Kajubi Mukajanga, Fili Karashani, Aboubakar Karsan, Nyaronyo Kicheere, Allan Lawa, Ally Saleh, Said Dogoli, Deo Mfugale, Moses Mataba, Mnaku Mbani.... orodha kamili inakuja. Maggid Mjengwa, Morogoro. Ijumaa, Januari 6, 2012.