Adverts

Jan 2, 2012

NMB MBEYA YATOA MISAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO MBEYA

Mkuu wa wilaya ya mbeya Evansi Balama akipokea msaada mafuta ya kupikia mahindi na maharage toka kwa meneja wa NMB tawi la mbalizi Bw.Nazareth Lebbi kwa niaba ya NMB makao makuu na kumwakilisha meneja wa kanda ya nyanda za juu kusini
Akikabidhi msaada hauo Meneja wa Benki hiyo Bwana Nazareth Lebi, mbele ya Mkuu wa wilaya ya Mbeya Bwana Evans Balama na Mbunge wa Mbeya mjini Bwana Joseph Mbilinyi, amesema msaada huo umegharimu shilingi milioni 10 za kitanzania na kwamba benki yake inawathamini na kuwajali wateja wake.
Mkuu wa wilaya Mbeya Bwana Evansi Balama akipokea msaada huo ameishukuru benki hiyo kwa moyo wa uzalendo wa kuwajali wateja wake na kuusema ni taasisi ya kwanza ya kifedha kutoa msaada huo
NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini imetoa misaada ya maguni 112 ya mahindi, maharage magunia 23 na mafuta ya alizeti lita 300, kwa waathirika wa mafuriko wa mtaa wa Ikuti Kata ya Iyunga jijini Mbeya mbeya yetu: source.