Adverts

Jan 18, 2012

TANGAZO KUTOKA WIZARA YA MALIASILI

UTARATIBU WA KUVUNA MAZAO YA MISITU KATIKA MASHAMBA YA MITI NA MASHARTI YA KUFANYA BIASHARA YA MAZAO YA MISITU NCHINI MWAKA WA FEDHA 2012/2013:
1.0 UTARATIBU WA KUOMBA KIBALI CHA KUVUNA MITI
1.1 Watu binafsi
i. Mwombaji atajaza fomu maalum ambayo itaambatana na picha.
ii. Fomu hiyo itapatikana katika ofisi za mashamba ya miti na katika mtandao wa Wizara
ambao ni www.mnrt.go.tz
iii. Muda wa maombi ni kuanzia February hadi 30 April ya kila mwaka
1.2 Makampuni/Biashara zilizosajiliwa
i. -Mwombaji atajaza fomu maalum ambayo itaambatishwa na nakala ya hati ya usajili ya
kampuni na picha ya mmoja wa wakurugenzi wa kampuni.
ii. -fomu itaambatishwa na nakala ya hati ya makubaliano ya biashara ya kampuni (
Memorandum of the company)
iii. -Fomu itapatikana katika ofisi za mashamba ya miti na katika mtandao wa Wizara ambao
ni www. mnrt.go.tz
iv. -Muda wa maombi ni kuanzia February hadi 30 April ya kila mwaka.
1.3 Vijiji vinavyopakana na mashamba ya miti
Vijiji vinavyopakana na mashamba ya miti yanayovunwa vitaandaliwa utaratibu wa
kunufaika na mapato yatokanayo na uvunaji wa mashamba hayo. Utaratibu huo utakuwa na
mikataba itakayowekwa baina ya Vijiji na Wakala wa Huduma za Misitu.
2.0 SIFA ZA MWOMBAJI
2.1 Waombaji binafsi
i. -Awe raia mwema wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 au zaidi
ii. -Awe na ushahidi wa uzoefu katika biashara nyingine yoyote
iii. -Kwa waombaji wanaoendelea wawe na ushahidi wa kulipa kodi toka Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA)
iv. -Mwombaji anayejishughulisha na upandaji miti atapewa kipaumbele
v. Awe na mchanganuo wa biashara
2.2 Makampuni na biashara zilizosajiliwa
i. -Kampuni iwe imesajiliwa na msajili wa makampuni Tanzania (BRELLA).
ii. -Iwe na uthibitisho wa ulipaji kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
iii. -Kampuni ijulikane mahali ilipo Tanzania bara (Physical address)
iv. -Kampuni zinazojishughulisha na upandaji miti zitapewa kipaumbele
v. Iwe na mchanganuo wa biashara inayofanya (Bussiness plan)
3.0 MASHARTI YA KUFANYA BIASHARA YA MAZAO YA MISITU NDANI YA
NCHI
i. Hati ya usajili kwa ajili ya biashara ya mazao ya misitu husika.
ii. Leseni ya biashara ya mazao ya misitu kutoka wilaya husika.
iii. Uthibitisho wa mlipa kodi yaani Tax Payer Identification Number (TIN).
iv. Wafanyabiashara binafsi wawe na uthibitisho wa kulipa kodi (Tax clearance certificate)
v. Kampuni iwe na uthibitisho wa taarifa ya hesabu za fedha kwa ajili ya biashara hiyo ambayo
imekaguliwa na kugongwa muhuri na wakaguzi wa mahesabu (Audited Financial returns) za
mwaka uliopita (A Copy of Statement of Business Returns done during the previous year and
Certified by Auditors).
vi. Kampuni itakayopata kibali cha uvunaji itaruhusiwa kuendelea na taratibu nyingine za
uwekezaji kama kupata ‘certifícate of incentives”
4.0 MASHARTI YA KUFANYA BIASHARA YA MAZAO YA MISITU NJE YA NCHI
Wafanyabiashara wanaosafirisha mazao ya misitu nje ya nchi, ni lazima waonyeshe vitu
vifuatavyo:
i. Hati ya usajili kwa ajili ya biashara ya mazao ya misitu husika.
ii. Leseni ya biashara ya mazao ya misitu kutoka wilaya husika.
iii. Uthibitisho wa mlipa kodi yaani Tax Identification Number (TIN).
iv. Nakala ya cheti cha mlipa kodi (Copy of the Income Tax Clearing Certificate);
v. Nakala ya maombi ya kutaka kununua bidhaa hiyo toka kwa muhusika aliye nje ya nchi
ikionyesha makubaliano ya malipo katika fedha za kigeni kama US Dollar au fedha ya
kigeni yoyote inayokubalika kwa meta za jazo wa mbao (Copy of order of enquiry from your
importer indicating tentative prices agreed in USD or any other International Convertible
currency per unit volume or quantity).
vi. Taarifa ya hesabu za fedha kwa ajili ya biashara hiyo ambayo imedhibitishwa na kugongwa
muhuri na benki ya mhusika (A Copy of Statement of Export Returns done during the year
and Certified by your Bankers (This applies to applicants wishing to renew their export
permit))
vii.Mwombaji awe amejisali katika Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ajili ya biashara ya
mazao ya misitu husika (A copy of Certificate of Registration from The Ministry of Natural
Resources and Tourism to deal with or trade in forest produce).
viii. Wafanyabiashara wanaoingiza mbao za misitu toka nje ya nchi, watatakiwa kujisajili na
mbao zote zitakazoingizwa nchini toka nje ya nchi zitatozwa ushuru wa kuingiza mbao hizo
nchini kwa kila meta ishirini za ujazo wa mbao hizo.
5.0 SIFA ZA VIWANDA VYA KUCHAKATA MAGOGO
5.1 Mashine/viwanda vitakavyoruhusiwa ni vile vyenye ubora katika uzalishaji wa mbao
(recovery rate) kuanzia asilimia arobaini ( 40%). Mashine/viwanda hivyo viwe na sifa
zifuatazo.
i) Sehemu tatu ambazo ni “Breakdown, Resaw na Edger”
ii) Wataalam wa aina tatu ambao ni Fundi Misumeno (Saw Doctor), Fundi Mwendesha
Mashine ya kupasa mbao (Trained Operator) na Fundi wa Matengenezo ya Mitambo
(Maintenance Technician/Manager).
iii) Viwanda vyote vitasimikwa nje ya msitu wa hifadhi
iv) Kiwanda kiwe na miadi ya kisheria kati yake na Serikali (Legal commitments) katika
kukigawia malighafi.
Nb: Leseni ya kusimika na kuendesha viwanda vya kuchakata mazao ya misitu kutoka Wizara
ya Maliasili na Utalii. Mwombaji atalipia ada kwa ajili ya kusimika kiwanda hicho;