Wakuu salamuni.
Baada ya kusoma michango ya wadau mabalimbali katika uzi huu http://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/207732-kwa-akinamama-tu-na-wababa-wazoefu.html, baada ya kutafuta na vyanzo vingine vya suala husika nje ya JF, ushauri msimamo na ushauri wangui ni huu hapa.
(I) Nawashukuru wote waliochangia, lakini pia niwashukuru zaidi walioshauri tusubiri mpaka atleast 2 months ndo tuanze kufahamiana na wife. Nawashukuru sana kwa ushauri huo.
(ii) Ni nyongeza ya kiimani juu ya suala husika.
Kwa mjibu wa BIBLIA, mwanamke aliyejifungua lazima akae hali ametenngwa kwa mda wa siku saba. Siku ya nane, kama amezaa mtoto mme, anatakiwa ampeleke kwa utakaso, atahiriwe nyama ya govi lake, baada ya hapo akae kwa mda wa siku 33 bila kufanya lolote wala kukutana na mwanamme.
Na kama ni mtoto wa kike, mwanamke anatakiwa akae hali ya kutengwa kwa wiki mbili, baada ya hapo ampeleke kutakaswa kisha akae bila kufanya chochote hasa kujamiana kwa mda wa siku 66. Haya yote yanapatikana WALAWI 12:1-10.
UZAZI WA MPANGO.
Kwa mjibu wa Biblia, njia za uzazi wa mpango tunazozitumia hivi leo, ni kukosoa njia aliyoianzisha MUNGU, kama unaamini. Hivyo, kwa muamini, ni mwiko kutumia uzazi wa mpango nje ya utaratibu wa MUNGU.
Iwapo mtu atakaa kwa mda wa siku zilizoamriwa kujitenga na mke/mme wake kwa mda ulioamriwa na MUNGU, mwanamke akawa ananyonyesha full time, basi homoni zinazowajibika kutengeneza mayai kwa ajili ya urutubishaji, zitaacha kazi hiyo na kujikita kutengeneza maziwa ya mtoto. Hivyo baada ya hapo, hakuna haja ya kutumia kondomu wala njia yoyote ile kwani MUNGU kesaha maliza hesabu zake tayari mpaka mtoto afikishe miaka miwili hadi mitatu.
Utata ulioopo ni kwa kizazi cha leo ambapo mama naye anawajibika kufanya kazi ili kuongeza lishe ya nyumbani, lakini kwa serikalini ndio maana hupewa likizo ya uzazi takribani siku 90 ili kuwezesha suala hilo kufanikiwa.
Mie nimeaacha kabisa, na najuta kwa nini sikufahamu suala hili mapema, hata hivyo najilaumu kwani yawezekana mazingira ya ndoa yangu ndiyo yaliyosababisha yote haya, kama ningehudhuria mafunzo ya ndoa kanisani yawezekana yasingenikuta haya.
Ebrania 13:4 "... ndoa na iheshimiwe na watu wote, na yawepo malazi safi kwa kuwa wazinzi na waasherati, atawahukumia adhabu....". Kwa mjibu wa andiko hili, ndiyo chanzo cha neno linalotumika KUBEMENDA. Kwamba iwapo mtu akifanya ngono nje ya ndoa yake, madhara ya ngono humpata mtoto aliyezaliwa, na kama hakutibiwa anaweza kufa.
Nawashukuruni sana.