Na Magreth
Sikambale
Mafunzo ya awali ya Mgambo yaliyodumu kwa kipindi cha
miezi mitatu yakishirikisha vijana 80 kutoka kata za Iyula na Ruanda wilayani
Mbozi ,yamefungwa rasmi leo na Ruteni kanali Emanuel Mwikuka.
Akifunga mafunzo hayo, Kanali Mwikuka ametoa wito kwa
vijana nchini kujtokeza na kushiriki katika mafunzo hayo ili kuimarisha ulinzi na
usalama wa Taifa na wanchi wenzao ujumla.
Alisema hayo wakati akijibu risala ya washiriki hao
iliyoeleza kuwa vijana wengi wamekua wakikwepa kujiunga na mafunzo hayo kwa
dhana kuwa mafunzo hayo ni mateso na hayana umuhimu kwao.
Kanali Mwikuka amesema, mafunzo hayo hayataishia hapo bali kutakuwepo
kozi nyingine kwa wale walio fuzu.
Ameongeza kuwa lengo la kuweka msukumo kwenye mafunzo hayo ni kwa ajili ya kuimarisha
ulinzi, na kwamba jeshi lina mpango wa
kuondoa wananchi walio ajiliwa katika sekta ya ulinzi ambao hawajafuzu mafunzo ya Mgambo na badala yake nafasi zao zitachukuliwa na
waliohitimu mafunzo ya mgambo.
“vijana mtakuwa
na nafasi kubwa yakupata ajira katika
ngazi za Serikali na Sekta binafsi” aliongeza Kanali Mwikuka.
Sambamba na hayo pia aliweza kuwatunuku vyeti
washiriki wa 5 waliyofanya vizuri katika mafunzo hayo Rebeka Mbembela, Jonas
Mgala, Musa Mgala, Heneriko Shonde, na mwile Stanlesi.
Katika risala iliyosomwa na Elia Japhet, wahitimu hao
walieleza kuwa mafunzo yao yalianza mwezi Julai mwaka huu na kwamba walianza mafunzo
hayo ni 120 hata hivyo kutokana na sababu mbalimbali washiriki 40 waliishia
njiani.
Mbali na hayo taarifa fupi
ilisomwa na mshauri wa mgambo wa wilaya ambapo amesema vijana hao
wameweza kujifunza mambo muhimu yanayotakiwa kufundishwa katika mafunzo ikiwemo
elimu juu ya rushwa toka Takukuru, ulinzi na usalama wa nchi.
Katika Maadhimisho hayo Kanali Mwikuka pia alikagua gwaride la wahitimu wa mgambo kabla ya kuwatunuku zawadi washindi mbalimbali.