Adverts

Jan 10, 2013

Deogratius Kisandu Apewa Kazi ya Kufanya NCCR-Mageuzi


SHUKRANI KWA KUTEULIWA(Deogratius Kisandu wakati ikipokea Kadi ya NCCR-Mageuzi. Kulia kwake ni Kaimu Katibu Mkuu Ndugu Faustin Sungura)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

YAH: SHUKRANI KWA KUTEULIWAKwanza natoa shukurani zangu za dhati, kwa Katibu Mkuu wa Kitengo cha Vijana wa NCCR-Mageuzi Ndugu Ojung Seitabau, kuniteua kuwa Katibu wa Mahusiano na Uenezi Taifa, kitengo cha vijana.

Baada ya uteuzi huu wa heshima kwangu, ninaahidi kwamba nitafanya kazi kwa kushirikiana na wenzangu ili kutimiza azma yetu na kutekeleza malengo yafuatayo:-1. Kuendeleza kauli mbiu ya vijana ya "VIJANA NI RASILIMALI YA TAIFA"

lengo kuu ni kuwasha indiketa kwa vijana kwamba milango sasa iko wazi

katika kulitumikia Taifa, na kazi ya ukombozi wa pili wa Taifa hili iko

mokononi mwetu, na tusikubali kufanya maandamano ambayo hatujui malengo yake na au hatukuyaandaa pamoja.2. Kuandaa baadhi ya wagombea vijana wa Ubunge na Udiwani kwa mwaka 2015 kupitia idara ya vijana nchi nzima.3. Kufanya uhamasishaji wa chama katika majimbo yote kwa nchi nzima.

4. Kuimarisha TASK FORCE YA USHINDI kwa vijana katika jimbo tutakayogombea .Ahsanteni Sana,

Deogratius Kisandu

KATIBU WA MAHUSIANO NA UENEZI TAIFA, KITENGO CHA VIJANA WA NCCR-Mageuzi

10/01/2013