Adverts

Jan 11, 2013

MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MAPINDUZI ZANZIBAR YAKAMILIKA


 

'Watoto
wa Kazi' Kikosi Maalum cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania { JWTZ },
Kikionyesha umahiri wake ndani ya Uwanja wa amani wakijiandaa na sherehe
za maapinduzi zinazofanyika kesho Jumamosi Tarehe 12 Januri 2013,
katika uwanja huo. Msanii
wa Kikundi cha Utamaduni cha Hiari ya Moyo kutoka Mkoani Domoma
kikipasha moto kujiandaa na utoaji burdani kwenye sherehe za
maaadhimisho ya kutimia miaka 49 ya mapinduzi ya Zanzibar zitakazofikia
kilele chake januari 12 2013.
  Kikundi
cha Utamaduni ya mchanga mdogo kisiwani Pemba kikitoa burdani ya ngoma
ya msewe katika matayarisho ya maadhimisho ya sherehe za kutimia Mikaka
49 ya Mapinduzi ya Zanzibar hapo Uwanja wa Amani. Kamanda
wa Brigedia nyuki Brigedia General Sharif Sheikh, akiwa pamoja na
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif, wakifurahia mwenendo
mzima wa matayarisho ya gwaride
  la Vikosi vya Ulinzi yaliyokuwa yakifanyika katika uwanja wa amani MJINI Zanzibar.


 Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya Taifa
ya sherehe na mapambo Balozi seif, akiwa na Waziri wake Kulia Mh. Mohd
Aboud Mohd na Kamanda wa Brigedia Nyuki Brigedia General Shjarif Sheikh
wakiangalia matayarisho ya mkwisho ya gwaride la sherehe za mapinduzi
katika uwanja wa amani Mjini Zanzibar.
----
Wakati
harakati za shamra shamra za maadhimisho ya kutimia miaka 49 ya
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964 zikikaribia kufikia
kileleni matayarisho ya mwisho ya gwaride la kuhitimisha sherehe hizo
zimekamilika rasmi.

Matayarisho  ya
Gwaride hilo ambalo ndilo linalopamba maadhimisho ya sherehe hizo za
Mapinduzi ya Zanzibar yamefanyika katika uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.

Mwenyekiti
wa Kamati ya Taifa ya sherehe na Mapambo ambaye pia ni Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa na Wajumbe wa Kamati hiyo
pamoja na Baadhi ya maafisa wa Vikosi vya ulinzi walishuhudia
matayarisho hayo.

Vikosi
vya ulinzi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania { JWTZ } Polisi, KMKM,
Mafunzo, JKU, Valantia na Zimamoto na uokozi vilianikiza ndani ya uwanja
wa Amani wakati  vilipokuwa vikitoa burdani ya gwaride la aina yake vikiongozwa na Vikosi vya Bendi.

Wakipita
mbele ya mwenyekiti huyo wa Sherehe na Mapambo Balozi Seif Askari hao
walionekana kuwa katika hali ya ukakamavu baada ya kufanya mazoezi ya
pamoja kwa kipindi cha mwezi Mmoja.

Staili
ya mwendo wa pole na ule wa haraka zikimalizia kwa heshima mbele ya
Viongozi hao ilionekana kukubalika vyema na walioshuhudia matayarisho
hayo kutokana na makofi ya vigeregere wakati wakitoa heshima zao.

Raha
zaidi ilionekana kuwakonga moyo walioshuhudia zoezi hilo wakati
maafandi hao walipomalizia kwa hatua 15 zilizofuatiwa na ule wimbo
maarufu unaomuhusu kila mwanafunzi anayepata elimu ya dunia katika
maskuli wa sisi sote tumegomboka.

Matayarisho
hayo yalifuatiwa na burdani za vikundi vya utamaduni vya Msewe kutoka
Mchanga mdogo Kisiwani Pemba, Mkunguru kutoka Kaskazini Unguja na Hiari
ya Moyo kutoka Mkoa wa Dodoma Tanzania Bara sambamba na Vijana wa
halaiki kutoka Skuli ya Sekondari ya Nyerere.

Akizungumza
na Wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Sherehe Zanzibar mara baada ya
kumalizika kwa matayarisho ya Gwaride hilo Mwenyekiti wa Kamati hiyo
Balozi Seif Ali Iddi amewashukuru na kuwapongeza Makamanda na askari wa
vikosi vya ulinzi kwa juhudi zao za matayarisho makini.

Balozi
Seif alielezea matumaini yake kutokana na matayarisho hayo kwamba
sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia Miaka 49 mwaka huu zitakuwa
nzuri na za aina yake.

Wakichangia
kwenye kikao hicho cha mwisho baadhi ya wajumbe wa Kamati hayo
wamewaomba wanachi watakaobahatia kuingia katika uwanja wa sherehe
waache kuchukuwa mikoba ambayo inaweza kuwaletea usumbufu wakati
wanapotaka kuingia uwanjani hapo.

Hata
hivyo wajumbe hao wamependekeza kwamba kikundi au taasisi itakayopangwa
kwa tukio lolote kiwanjani hapo wakati wa sherehe hizo wakazingatia
zaidi wakati ili kwenda vizuri na ratiba iliyopangwa.
NaOthman Khamis AmeOfisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar