Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Mwanaidi Maajar (wapili toka kulia)akiingia nyumbani kwa Balozi wa Nigeria (hayupo pichani) Potomac, Maryland, huku wakipokelewa na afisa ubalozi wa Nigeria (wa kwanza kulia) anayesalimia ni mama Lily Munanka ambaye ni mkuu wa utawala na fedha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani akifuatiwa na mume wa Balozi, Bwn. Shariff Maajar siku ya Jumapili January 6, 2013 siku Balozi wa Nigeria alipomfanyia chakula cha jioni maalum kwa ajili ya kumuaga Balozi wetu ambaye anamaliza muda wake.
Mhe. Mwanaidi Maajar akilakiwa na Balozi wa Nigeria nchini Marekani, Mhe.Adebowale Ibidpo Adefuye siku ya Jumapili January 6, 2013 alipomfanyia chakula cha jioni maalum kwa ajili ya kumuaga Balozi wa Tanzania nchini Marekani ambaye anamaliza muda wake.
Mke wa Balozi wa Nigeria akisalimiana na kumkaribisha Mhe. Mwanaidi Maajar huku mumewe Bwn. Shariff Maajar akiwa amesimama kwenye ngazi akiangalia.
Balozi na mumewe Bwn. Shariff Maajar wakisalimiana na Rais wa Jumuiya ya Watnzania DMV, Bwn Idd Sandaly ambaye pia aliongozana na mkewe (wakwanza kushoto) kwenye chakula cha jioni alichoandaliwa Balozi wetu na Balozi wa Nigeria kwa ajili ya kumuaga siku ya Jumapili January 6, 2013 nyumbani kwake Potomac, Maryland.
Kutoka kushoo ni Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV akiwa pamoja na mkewe, Balozi wa Benin nchini Marekani Mhe.Cyrille S. Oguin katika picha ya pamoja na Balozi wa Nigeria nchini Marekani Mhe.Adebowale Ibidpo Adefuye.
Balozi wa Nigeria nchini Marekani Mhe.Adebowale Ibidpo Adefuye (kulia) akisalimiana na Mume wa Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Bwn. Shariff Maajar.
Balozi wa Botswana nchini Marekani Mhe. Tebelelo Seretse (kushoto) akiongea jambo na Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Mwanaidi Maajar.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Utawala na Fedha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, mama Lily Munanka, Mke wa Balozi wa Zimbabwe, Balozi wa Zimbabwe nchini Marekani, Mhe. Dr. Machivenyika Mapuranga na Balozi wa Benin nchini Marekani Mhe. Cyrille S. Oguin.
Wakati wa chakula
kwa picha zaidi bofya read more
kutoka blog ya VIJIMAMBO