Basi la Taqwa lililokuwa safarini nchini Zambia limegongana na roli na kuua watu watatu papo hapo.
kulingana na radio One ya nchini Zambia ajali hiyo imetokea eneo la wilaya ya Shiwang'andu katika jimbo la Muchinga leo jioni na kuhusisha basi lenye namba za usajili T 298 BLZ lililokuwa linatokea Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo ambapo limegongana na roli pia mali ya nchini Tanzania
katika ajali hiyo watu watatu wamefariki akiwemo dereva wa basi OSWARD DAISON MWAWAPA na Konda wake Mapinduzi Gilbert Siwale na abiria mmoja ambaye hajatambuliwa na maiti zao zimehifadhiwa hospitali ya Chansali nchini Zambia.
Abiria wengine watano waliokuwa kwenye basi la Taqwa ambao ni majeruhi wamelazwa kwenye hospitali ya wilaya ya Chinsali nchini humo.
Mkuu wa polisi jimbo la Munchinga Kamishna wa polisi Remmy Kajoba na Katibu msaidizi wa jimbo la Munchinga Jewis Chabi wamethibitisha kutokea kwa ajali hiyo kwa njia ya simu.
Roli lilohusika kwenye ajali hilo lina namba za usajiri T302 BBR lenye tela lake lenye namba T453 AHP lililokuwa likitokea Lusaka ambapo ajali imetokea majira ya saa 10.30 (ya zambia) sawa na 11.30 ya Tanzania, katika kijiji cha Chikumba kilometa 29 kutoka makao makuu ya wilaya ya SHIWANG'ANDU
Kulingana na taarifa hizo dereva wa roli alikuwa akijaribu kulipitia roli na kuligonga trela la roli na hivyo kubingilika upande wa kushoto
Bus hilo lilikuwa na shehena ya mizigo kutoka Kongo na kulikuwa na abiria 11 tu wakati roli hilo likitokea Lusaka lilikuwa halina mzigo
Naibu Katibu wa jimbo huyo amewataka ndugu na jamaa kutoka nchini Tanzania kwenda kutambua maiti moja ambayo haijatambuliwa na pia ndugu wa marehemu waliotambuliwa ili kuchukua maiti zao
aidha mwanamke mmoja majeruhi bado hali yake ni mbaya na imeelezwa kuwa ni mtanzania pia ambaye jina lake halijapatikana wakti majeruhi wanne hali zao zinaendelea vyema
mwisho