Adverts

Feb 25, 2013

MAGEREZA HOI MBELE YA AFYA, YALALA 3-2

TIMU YA MAGEREZA MBOZI AMBAYO JUZI ILIAMBULIA KICHAPO CHA MABAO 3-2 KATIKA MCHEZO WA KIRAFIKI KATI YAKE NA AFYA (HOSPITALI YA MBOZI)
 MOJA YA MAJARIBIO YA TIMU YA AFYA  KUINGIA KWENYE 18 ZA TIMU YA MAGEREZA
 CHIEF AKIWA HANA HAMU BAADA YA KUKUBALI KICHAPO KWA TIMU YAKE
HIKI NDICHO KIKOSI CHA MAANGAMIZI CHA HOSPITALI YA WILAYA MBOZI KILICHOWALOPOA MAGEREZA BAO 3-2 KATIKA UWANJA WAO WA NYUMBANI

Na Mwandishi wetu

Timu ya Magereza Mbozi jana imeonja joto ya jiwe baada ya kubamizwa mabao 3-2 katika mchezo wa kirafiki na Hospitali ya wilaya Mbozi
Katika mchezo huo uliovuta mashabiki  ulifanyika katika uwanja wa magereza Mbozi ambapo hadi mapumziko Hospitali ya wilaya Mbozi ilikuwa mbele kwa bao 2-0
Kipindi cha pili kilianza kwa kufanya mabadiliko kadhaa kwa timu ya Magereza ambapo hatua hiyo iliwezesha kuleta uhai kwa timu hiyo na kujipatia bao la kwanza dakika ya 64.
Dakika chache baadaye timu ya Hospitali ilijipatia bao la 3 na hivyo kuonekana kuwamaliza kabisa nguvu maafande wa magereza. Hata hivyo zikiwa zimebakia dakika chache, magereza walipata bao la pili na hivyo kuufanya mchezo kumalizika kwa Hospitali kutoka uwanjani wakiwa wamenenepa kwa ushindiw  bao 3-2.