MBOZI
12, FEB 2013 HUKUMU
Mahakama kuu kanda ya Mbeya
imemhukumu PETER MWAFRIKA mkazi wa Ndolezi wilayani Mbozi kunyongwa
hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kuua kwa kukusudia.
Akisoma hukumu hiyo iliyochukua saa
1.30 Jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya mbeya NOEL CHOCHA amesema
licha ya mikono ya mahakama kufungwa kutoa adhabu ndogo kwa kosa la maauaji ya
kukusudia, pia adhabu hiyo ni hatua ya kukomesha watu wenye tabia kama za
mtuhumiwa kujichukulia hatua mikononi mwao.
Akirejea mazingira ya kesi hiyo jaji
Chocha amesema mnamo Februaly 11,2010 mshatakiwa na wenzake watatu walifanya
kosa la mauaji ya kukudia chini ya kifungu 196 chasheria ya mwenendo wa makosa
ya jinai kwa kumuua KOSAM MWAFRIKA ambaye ni kaka wa marehemu
katika kijiji cha Shaji kwa kumkata koromeo na kulitenganisha vipande viwili.
Jaji Chocha katika maelezo yake
alisema mshtakiwa akiwa na wenzake ambao walitoweka baada ya mauaji hayo
walimvamia Kosam akiwa na mkewe shambani kwake eneo la Zanzule, Ndolezi na
kisha kumkamata marehemu kwa maelezo kuwa walikuwa wametumwa kumkamata ili
wampeleke polisi kwa kosa la wizi wa Ng'ombe.
Hata hivyo katika mabishano shambani
hapo, marehemu na wenzake walitamka wazi kuwa walikuwa wametumwa kumuua
marehemu hivyo kuongeza nguvu za ushahidi wa kumtia hatiani.
sababu za mauaji hayo ni ugomvi wa
muda mrefu uliokuwepo kati ya marehemu na mama yake mzazi wa mshtakiwa ambao
walikuwa wakigombea ardhi,(wote ni ndugu) na kwamba siku moja kabla ya tukio
hilo kulikuwa na kesi katika mahakama ya mwanzo Mlowo iliyokuwa imefunguliwa na
Mama mzazi wa mshatakiwa.
Inaelezwa pia kuwa wakiwa njiani
kumpeleka polisi, baada ya kubaini kuwa kuna watu wanawafuatilia ghafla
mtuhumiwa mwingine (ambaye hakuwepo mahakamani) alimkata marehemu panga la
shingo na kumfanya marehemu akose nguvu na kuanguka, hata hivyo kwa kuonyesha
kutoridhika na hali hiyo mtuhumiwa aliongezea kwa kumkata marehemu na panga
kwenye koromeo na kulitenganisha kabisa.
Jaji kabla ya kutoa hukumu alirejea
mazingira ya tukio hilo na kujiridhisha na miongozo, viini vya shauri la mauaji
na hoja zilizotolewa na washauri wa mahakama ambapo ilithitika kuwa kulikuwa na
dhamira ya mauaji na tendo la mauaji lilifanyika
Katika ushahidi wa shauri hilo jumla
ya mashahidi watatu waliletwa mahakamani akiwemo kaka wa mshtakiwa ambao wawili
kati yao walithibitisha pasipo shaka kwamba mshtakiwa Peter kuhusika na
tukio la kumuua kwakukusudia Kosam .
Katika utetezi wake wakili wa
mshtakiwa ZAKIA SULEIMAN aliiomba mahakama impe adhabu nafuu mshtakiwa kutokana
na umri wake mdogo hivyo mchango wake kuhitajika katika ujenzi wa taifa, pamoja
na kuwa na wategemezi wakiwemo wake wawili na watoto wane.
Serikali iliwakilishwa na Wakili
Rogers Francis
katika hatua nyingine jaji Chocha
aliamua kufanya kazi ya kutoa elimu mahakamani humo, akirejea matukio
yaliyojitokeza hivi karibuni wilayani Momba na Mbozi aliyoyaita ni yanafanywa
na watu wasiopenda ama hawana habari na Utawala wa sheria yakiwemo kuwazika
watu wakiwa hai, ambapo amesisitiza hali hii inaonyesha kuwepo kwa watu
waliovuka kiwango cha ukatiri katika jamii.
amesema hali ya kushamiri mauaji
wilaya za Mbozi na Momba kuhaonyesha namna jamii na watu wenye tabia kama
za mshitakiwa wasivyopaswa kuvumilika mbele ya sheria na kwamba adhabu hiyo
itasaidia kuwaelimisha wengine wenye mitazamo kama ya mshtakiwa Peter Mwafrika.