Adverts

Feb 9, 2013

MOMBA NA MBOZI ZAGAWANYWA, SASA YAWA MABARAZA MAWILI YA MADIWANI

 Hatimaye safari ya miaka 10 ya kuhitaji wilaya Mbili ndani ya Mbozi imefikia tamati leo baada ya mkuu wa mkoa wa Mbeya kukabidhi cheti cha ukubalifu wa kuanzishwa kwa mamlaka ya halmashauri ya wilaya ya Momba .
Cheti hicho kinaonyesha mipaka na maeneo ya wilaya hiyo kimekabidhiwa kwa mkuu wa wilaya ya Momba ABIUD SAIDEA ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa na kiu ya kugawiwa eneo lake la utawala na watumishi tangu kutangaza kuanzishwa kwa wilaya hiyo.

Katika hatua ya kuonyesha kugawanywa kwa wilaya hizo, baraza la madiwani lililivunjika na kufanyika uchaguzi kwa halmashauri ya Mbozi na Momba ambapo kwa upande wa Mbozi nafasi ya Makamu mwenyekiti imechukuliwa na Diwani Allan Mgullah na Kwa upande wa Momba mwenyekiti wa halmashauri amechaguliwa Mh Bernard Sichilongwa
 BARAZA LA MADIWANI LA MOMBA LIKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MKUU WA MKOA MBEYA  NA MZEE ELIACHIM SIMPASA AMBAYE NDIYE MWANZILISHI WA MCHAKATO WA KUGAWA WILAYA MBILI ZA MBOZI
 BARAZA LA MADIWANI WA HALMASHAURI YA MBOZI LIKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MKUU WA MKOA WA MBEYA ABAS KANDORO
 BARAZA LA MADIWANI KABLA HALIJAVUNJWA ASUBUHI YA LEO - HII NDIYO PICHA YA LALA SALAMA YA HALMASHAURI YA MBOZI AMBAYE HATIMAYE ZIMEKUWA MOMBA NA MBOZI
 MKUU WA WILAYA YA MOMBA ABIUD SAIDEA AKIWA AMESHIKIRIA HATI YA KUANZISHWA HALMASHAURI YA WILAYA YA MOMBA
MKUU WA MKOA WA MBEYA ABAS KANDORO AKIWA AMESHIKIRIA HATI YA MOMBA KABLA YA KUTANGAZA RASMI KUIGAWA KUTOKA ILIYOKUWA HALMASHAURI YA MBOZI NA SASA KUWA NA HALMASHAURI YA MOMBA NA MBOZI