HAPA NI BAADA YA KUFUNGULIWA KWA MABUCHA WANAYOYAITA YA WAKRISTO NA KUANZA KUUZA NYAMA KATIKA MJI WA TUNDUMA
PAMOJA NA HALI HIYO YA MVUTANO TUNDUMA SHUGHULI ZILIENDELEA KAMA KAWAIDA
SHEIKH WA WILAYA YA MOMBA AKIZUNGUMZIA HATUA YA MAANDAMANO YA VIJANA WA KIKRISTO AMBAPO AMEOMBA WATULIE KWAKUWA JAMBO HILO LIPO KWENYE MAZUNGUMZO
KIKUNDI CHA VIJANA WA KIKRISTO WAKIWA WAMEANDAMANA JANA MJINI TUNDUMA KUTAKA NYAMA WALIZOCHINJA ZIRUHUSIWE KUUZWA
KIKUNDI CHA VIJANA WAKIWA WAMEBEBA BIBLIA NA MFANO WA MSALABA WAKIANDAMANA KUSHINIKIZA NYAMA WALIZOKUWA WAMEZICHINJA SIKU YA JUMAMOSI ZIRUHUSIWE KUUZWA MABUCHANI

MOJA YA BUCHA ILIYOTANABAISHWA KWA IMANI KTIKA MJI WA TUNDUMA
Kikundi cha Waumini wa kikristo katika mji wa Tunduma mkoani Mbeya jana mchana kimeongoza maandamano kupinga hatua ya mkuu wa wilaya ya Momba Abiud Saidea kuzuia nyama iliyochinja na wakristo wenzao isiuzwe kwenye mabucha yao

Hatua hiyo ni matokeo ya maelekezo ya mkuu huyo wa wilaya
aliyoyatoa juzi kuwa nyama iliyochinjwa na wakristo kuzuiwa isigongwe mihuri na
afisa afya wa eneo hilo tayari kwa kuuzwa na badala yake kuruhusu nyama
iliyochinjwa na waislamu igongwe mihuri
na kuuzwa
Kutokana na hali hiyo watu waliochinja nyama hizo
wakajikusanya leo mchana baada ya
kubaini kuwa walikuwa wakielekea kupata hasara kutokana na tangazo hilo la serikali na hivyo kuamua kuandamana
hatua ambayo ikalazimu mkuu wa wilaya kubadili maamuzi na kuwataka wakauze nje
ya mji wa Tunduma.
Msimamo wa wauza bucha
ulikuwa nyama walizochinja waziuzie kwenye maduka yao ambayo wanafahamu
wazi wateja wao ni wakristo. Hali hii ilizua ugumu wa kutoa maamuzi hadi maandamano
yaliyoanza saa saba mchana kumsukuma afisa afya kugonga mihuri kwenye nyama
zilizochinjwa na wakristu jana na kuanza kuuzwa.
Hadi kamera yetu inatoka eneo la Tunduma, tayari walikuwa
wameshafikia mwafaka kuwa nyama iliyochinjwa na wakristo kwa mara ya kwanza
jana mjini Tunduma iuzwe lakini baada ya hapo utaratibu huo usimame mpaka
watapapofikia mwafaka katika majadiliano yanayoendelea baina ya viongozi wa
kikristo na waislamu pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya.
Sheikh mkuu wa wilaya ya Momba anayeishi katika mji wa Tunduma Ahmed Omary
anaeleza kuwa vikao vya kufikia
makubaliano ya suala la kuchinja baina ya waislamu na wakristu kwa kushirikiana
na uongozi wa wilaya bado vinaendelea hivyo ni vyema wananchi wakawaachia
viongozi hao ili wafikie makubaliano
Kutokana na hali hiyo hali ya mji wa Tunduma kwa jumapili ya
leo imekuwa katika hofu ingawa katika maandamano hayo hapakuambatana na vurugu
zozote ambapo waongoza maandamano walitengeneza mfano wa msalaba na biblia
vikitangulizwa mbele kwenye maandamano yao ingawa haijafahamika ililenga ujumbe
gani.
Katika siku ya jana kwa sehemu kubwa ujumbe umetolewa
makanisani kupitia waraka wa Tamko la muungano wa miamvuli ya makanisa
nchini TCF inayoshirikisha makanisa CCT,
TEC, PCT na Waadventist kutaka serikali iache kuvunja katiba kwa kuingilia
suala la uchinjaji na kuachia wakristo waendelee kujichinjia kwakuwa kuaachia
waislamu kuchinja ni sehemu ya kutekeleza ibada ya dini nyingine na hivyo kuingilia uhuru wa
kikatiba wa kuabudu
Waraka huo mrefu uliosomwa na viongozi wa makanisa hayo,
umegusia maeneo mbalimbali wanayoona serikali haijayatilia mkazo na kutaka
ichukue hatua katika hoja zake walizoziorodhesha.