Adverts

Sep 30, 2013

MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUTUMIA RUZUKU YA MINJINGU TU


MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUPATA RUKUZU YA MINJINGU TU
KILIO CHA WAKULIMA CHAPUUZWA!

Na Danny Tweve –Njombe

Asimilia 67.53 za kaya zote nchini zilizopewa ruzuku ya Mbolea ya
kupandia kwa mikoa 11 inayotegemewa kwenye uzalishaji wa mazao ya
chakula nchini zitapata mbolea ya Minjingu mazao  tofauti na
malalamiko ya wakulima wengi kwa mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe
kuhusiana na mbolea hiyo.

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo  imetoa maelekezo kwa makatibu
tawala mikoa ikieleza kuwa itafidia sehemu ya bei ya pembejeo kwa
mazao ya Mahindi na Mpunga kwa  kaya 932,100 katika wilaya 109 nchini
kwa msimu wa kilimo wa 20013/2014 unaoanza mwezi October mwaka huu.

Kulingana na waraka ulioelekezwa kwa makatibu tawala mikoa  ya
Tanzania bara  wa Septemba 12,2013 na kusainiwa na Katibu Mkuu wizara
hiyo Sophia Kaduma unaeleza kuwa ruzuku ya pembejeo kwa mwaka huu
itaelekezwa kwa mikoa 24 kwa Tanzania bara  huku ukitoa masharti kwa
mikoa 11 kupewa  mbolea ya minjingu mazao tu.

Mikoa 11 ambayo kaya zake 629,497 zitapaswa kutumia mbolea ya Minjingu mazao inahusisha wilaya za Mbozi, Makete, Njombe na Mbeya ambakokumekuwepo malalamiko ya kushindwa kwa Mbolea ya Minjingu kufanya kazi licha ya maboresho yaliyofanyika.

Waraka huo wenye kumbnukumbu Na AE.13/209/01 unalekeza kuwa kutakuwa na aina mbili za utoaji wa rukuzu ya pembejeo kwa wananchi ikiwemo utaratibu wa  vocha  ambao utachukua asilimia 80 ya ruzuku yote na sehemu iliyobakia itatumika utaatibu wa mikopo  ya pembejeo kupitia
vikundi vya wakulima vilivyosajiliwa na vyenye sifa  ya kukopesheka.

Aidha waraka huo unaelekeza bei elekezi za mbolea ya Minjingu mazao
kwa mikoa 11 ya Katavi, Kigoma, Mbeya, Njombe, Iringa, Rukwa, Ruvuma,
Morogoro, Dodoma , Tabora na Singida ambapo itauzwa katika ngazi ya
wilaya kwa bei ya shilingi 32,500/= kwa mfuko wa kilo 50(hamsini).

Kulingana na maelekezo hayo wakulima wa wilaya zilizokuwa zikipinga
matumizi ya mbolea ya Minjingu mazao  kwa mikoa inayopata ruzuku ya
pembejeo kutoka serikali ya Tanzania zitapaswa  kukubaliana namatumizi
ya mbolea hiyo isipokuwa kwa wilaya za mikoa 13 mingine ambayo inapata
ruzuku  ya serikali pamoja na benki ya dunia ambapo wakulima wanaweza
kuchagua Minjingu mazao ama aina nyingine ya mbolea.

Kulingana na maoni ya baadhi ya wakulima, hatua hiyo inaweza
kuwarejesha wakulima kwenye kilio cha miaka  michache iliyopita ambapo
matumizi ya Mbolea ya Minjingu hayakuonyesha mafanikio mashambani hali ambayo ililazimu serikali za wilaya na mikoa husika kutafakari upya
matumizi ya mbolea hiyo.

Mikoa 13 iliyopewa nafasi ya kuchagua  aina gani ya mbolea ya kupandia
baina ya minjingu mazao na DAP ni pamoja na Mara, Kagera, Mwanza,
Geita ,Shinyanga, Simiyu, Manyara, Arusha,Kilimanjaro, Tanga, Pwani,
Mtwara na Lindi.

Katika hatua nyingine wizara imeagiza pembejezo za ruzuku
zitakazofikishwa mikoani zinapaswa kuwasilishwa kwenye ngazi ya wilaya
katika kipindi cha saa 48 hatua ambayo inalenga kuepusha ucheleweshaji
na urasimu unaochangia malalamiko kwa wakulima