Na Danny Tweve Mbozi
Mjumbe wa kamati ya
Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji na Mbunge wa jimbo la Mwanakwerekwe Mh Haji
Jumaa Sereweji amesema kuna haja kwa wizara ya Kilimo kuipeleka kamati hiyo
kwenda kujifunza namna mvua za
kutengenezwa zinavyoweza kuleta ufanisi
Mbunge huyo akichangia
hoja iliyoanzishwa na Mbunge wa Rungwe magharibi Profesa David Mwakyusa kuwa
serikali ianze kubadilisha mfumo wa kusaidia maeneo yenye njaa kwa kupeleka
chakula na badala yake fedha zinazotengwa kwaajili ya kununua chakula cha akiba
zielekezwe kujenga miundombinu ya umwagiliaji kwa maeneo yenye ukame.
Mtendaji Mkuu wa wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula Bw. Charles Walwa akizungumza na wakulima na mawakala waliouza mahindi yao kwenye kituo cha Vwawa wilayani Mbozi |
Miongoni mwa zana za kuchambua uchafu wa mahindi yanayofikishwa kituoni hapo na wakulima kwa njia za udanganyifu kwa kuweka takataka kwenye magunia yao |
shenena ya mahindi ambayo inasubiri kusafirishwa kwenda Makambako na jijini Dar es salaam kutokana na maghala kutotoshereza wingi za mahindi yaliyopo |
Mtendaji wa NFRA BW. CHARLES WALWA akijibu hoja za kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji liyofanya ziara kwenye maghala ya Vwawa wilayani Mbozi ambako shehena kubwa imeanza kusafirishwa kupelekwa jijiji
sehemu ya shehena ya mahindi yaliyopo kwenye ghala la Vwawa
Wabunge wakihoji ubora wa magunia yanayotumika katika uhifadhi wa nafaka kwenye ghala la NFRA Vwawa Mbozi
Mbunge wa Sikonge Mh Said Nkumba akizungumza na wafanyabiashara, mawakala na wakulima waliouza mahindi yao kwa wakala wa hifadhi ya chakula ya Taifa NFRA katka kituo cha Vwawa ambapo wanalalamikia kucheleweshewa malipo yao
Ujumbe wa kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikiwasilishwa na mtendaji mkuu wa wakala NFRA |
Mh Sereweji alisema
yeye kwa mtazamo wake Tanzania ya sasa haipaswi kuendelea kusubiria umwagiliaji
wa kutegemea mvua za mwenyezi mungu ambazo zinaathiriwa na mabadiliko ya tabia
nchi, na kwamba ubunifu na matumizi ya teknolojia za umwagiliaji zaidi zikiwemo
mvua za kutengeneza
Ningeshauri kamati hii
ipelekwe kuleee wapi kule malasia ili ikajifunze na kuona ufanisi wa mvua hizo
ili teknolojia hiyo iletwe nchini na kutumika kwaajili ya kuongeza uhakika wa
chakula hasa kwa maeneo yenye ukame.
Akizungumza kwenye
ziara yao ya kushtukiza walioifanya kwenye ghala la kusafirishia nafaka la Wakala
wa hifadhi ya Taifa ya Chakula NFRA lililopo eneo la Vwawa wilayani Mbozi , Mbunge
wa Rungwe Magharibi Profesa David Mwakyusa alisema kuna baadhi ya maeneo nchini
yamejipa hati miliki ya misaada ya chakula kila msimu licha ya maeneo hayo kuwa
na fulsa zingine za uzalishaji.
Profesa Mwakyusa
alisema kuna umuhimu kwa maeneo hayo kuhamasishwa kuanzishwa mifumo ya
umwagiliaji ambayo itawezesha kufanya
umwagiliaji pale mvua za zinaposimama na kwamba fedha zinazotengwa kununua
nafaka zielekezwe kwenye miradi hiyo ya umwagiliaji.
Katika taarifa yake
Mtendaji Mkuu wa wakala wa hifadhi ya Chakula nchini NFRA Bwana Charles Walwa
alisema wakala yake imepokea kiasi cha shilingi Bilion 70 kwa mwaka wa fedha
2013/2014 kati ya Bilion 100 ilizozitarajia kwaaajili ya kulipa kwa wakulima na
mawakala kutokana na ununuzi wa nafaka
Alisema wakala yake ina
imani kuwa deni la bilioni 30.2 litalipwa mapema ili kuwezesha wakulima
kuendelea na hatua za maandalizi ya msimu ulioanza wa kilimo na kwamba wakulima
na mawakala wawe wavumilivu kwa muda mfupi huu ambao maalipo hayo yanaandaliwa
hazina.
Mtendaji huyo amesema
katika hatua za kuipunguzia gharama za uendeshaji, wakala hiyo inafanya
mazungumzo na makampuni ya hapa nchini kuanza kutengeneza mifuko ya visalfeti
kwaaajili ya kuhifadhi nafaka badala ya kutumia magunia ambayo bei zake
zimekuwa zikipanda msimu hadi msimu.
Alisema wakala imekuwa
ikitumia kiasi cha shilingi Bilion 5 kwa kila msimu kwaajili ya kununua magunia
ya katani kwa ajili ya kuhifadhi nafaka ambayo yamekuwa yakiharibika katika
kipindi kifupi tofauti na teknolojia ya visalfet ambayo inatumiwa na nchi
jirani kama Zambia ambayo imeonekana inapunguza gharama zaidi ya nusu ya ile
wanayotumia sasa.
Kwa upande wake Mwenyekiti
wa kamati ya Bunge inayosimamia Kilimo, Mifugo na Maji Mh SAID MKUMBA ameelezea kuridhishwa na jitihada za wakala
hiyo katika kujipanga kwaajili ya kujitegemea
Alisema hatua za sasa
za kuanza kujenga na kupanua maghala ni hatua muhimu ya kuonyesha uwezo wake
katika ukusanyaji wa mazao na kulipa kwa bei nzuri kwa wakulima.
Alisema kiwango cha
shilingi 500 kwa kilo kiliweza kuvutia wakulima wengi kuuza mazao yao kwa
NFRA hivyo hatua iliyobakia ni kuendelea
kujenga imani hiyo kwa wakulima kwa kuhakikisha wanalipwa kwa wakati ili
waendelee kushiriki uzalishaji kwa tija.
Kamati hiyo ya Bunge
ilizungumza pia na mawalaka na wakulima ambao wanaidai NFRA ambao miongoni mwao
walionyesha kuchoshwa na ahadi za malipo yaliyocheleweshwa yanayofikia Bilion
30.2kwa nchi nzima huku kiasi kikubwa kikiwa ni wakulima wa mikoa ya Mbeya na
Rukwa.
Mwisho