Adverts

Oct 13, 2013

MAUZA UZA YA DUNIA-KIJANA AMWOA MAMA YAKE MZAZI! RUVUMA

 Katika hali inayoonyesha dunia ipo Ukingoni kijana ajulikanaye kwa jina la Joseph Mapunda mkazi wa Mbinga mkoani Ruvuma amemweka kimada mama yake mzazi na kuendelea kushiriki naye tendo la ndoa kwa kipindi cha miaka 10 imefahamika.
Huyu ndiye Joseph Mapunda aliyemwoa mama yake mzazi 
 Katika hali ya kuonyesha dunia ipo ukingoni, kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Joseph Mapunda amefanya laana ya mwaka kwa kumuoa mama yake kwa kipindi cha miaka 10 hadi juzi alipoumbuliwa mbele ya mganga wa tiba za asili ajulikanaye kama Bibi Ndembo.
Tukio hilo ambalo kulingana na kipindi cha Kanjanja Time cha Channel Ten, limetokea mkoani Ruvuma katika wilaya ya Mbinga ambapo serikali ya kijiji inaangalia uwezekano wa kumkabidhi kijana huyo kwa mamlaka za dola ili achukuliwe hatua.
Kulingana na mahojiano na timu ya kanjanja time, kijana huyo Joseph Mapunda anasema kuwa alishaoa wake zake watatu lakini aliwaacha wote kutokana na kuwa na mapenzi zaidi na mamaye ambaye walianza kushirikiana tendo la ngono miaka kumi iliyopita.
Akizungumza pia mama Mapunda anaeleza kuwa alimweleza wazi mtoto wake huyo wa mwisho kuwa anampenda na anataka waoane jambo ambalo mwanaye huyo hakukataaa na wakaendelea kula maisha kama mke na mme.
Hata hivyo inadaiwa kuwa kulikuwa na mambo ya dunia ya tatu zaidi(ushirikina) katika masuala yao ya mahusiano na ndiyo sababu wananchi walipoona jambo hilo si la kawaida waliama kuliwasilisha kwa mganga wa tiba za asili Bi Ndembo ambaye aliwaita wote na kuwaweka hadharani
Anaeleza kuwa walinyolewa na ndipo wakaweza kutoa maelezo namna walivyojihusisha na ushirikina na pia ushirika wao wa mapenzi ulilenga kuiamrisha zaidi mtandao wao wa kiushirikina kama mama na mwana na mke na mme! Jambo ambalo lilidumu kwa miaka  kumi.
Akizungumza  baada ya kutolewa kwa mganga huyo Kijana Joseph Mapunda anaeleza  kuwa hatarudia tena kumfanya mama yake mkewe na kwamba akitaka kutii kiu yake atatafuta wa kumfurahisha na siyo mama yake tena.
Hata hivyo katika maelezo yake mama mtu anaeleza wazi kuwa hayupo tayari kukubali kuachana na bwana wake Joseph kwakuwa bado anampenda! Huku akizungumza lafudhi ya kingoni mama huyo anasisitiza kuwa anampenda mno Joseph kama bwana wake.
Naye Joseph baada ya mahojiano ya muda mrefu anasema” nitaangalia uwezekano wa kuachana na mama  kama mke wangu, ila najua ni suala gumu “
Mashuhuda wa  jambo hilo  akiwemo Bi Isabela Ponera anayeleza kuwa alifika kwa mganga huyo  Julai  3 mwaka huu na baadaye kukutana na kesi ya Joseph na Mama yake  ambayo yeye binafsi hajawahi kukutana na tukio kama hilo tangu azaliwe mwaka 1960!
Wengi wa waliohojiwa kuhusiana na tukio hilo wanapendekeza Joseph afungwe miaka kadhaa ili ajifunze kuwa ni kosa kufanya ngono na mama yake mzazi, angawa kwa upande wa mama Joseph ambaye anaonekana kuwa na umri mkubwa karibu miaka 70 wanamwonea huruma kuwa akifungwa anaweza kufia jela.

Huyu ni mamayake Joseph aliyeolewa na mwanaye  kwa kipindi cha miaka 10 huku akieleza kufurahia unyumba na mwanaye!!