Adverts

Oct 13, 2013

MWANDISHI MWINGINE AJERUHIWA KWA RISASI NA MAJAMBAZI MBOZI

Hili ndilo trekta liliwatia vishawishi majambazi hao na kudhani ndani kuna mamilioni na hivyo kumwekea mkakati wa kumvamia usiku, pembezoni mafundi wakirekebisha dirisha lililokuwa limevunjwa wakati fatuma lilipotupwa kwenye mlango wa bawna Mtaki na baadaye kutumia risasi kuvunja vitasa vya milango ya nyuumba hiyo kabla ya kuwajeruhi

Mmoja wa ndugu wa bwana Mtaki akimpa pole kutokana na uvamizi uliosababisha majeruhi kwa bwana Mtaki na mkewe ambapo mkewe amejeruhiwa maeneo ya mwili kuanzia tumboni hadi miguuni kutokana na baruti za gobole kumuunguza huku goroli zikibakia mwilini

Mkewe bwana Mtaki akilia wakati alipokuwa akitembelewa na ndugu jamaa na marafiki kumpa pole kutokana na tukio hilo la uvamizi wa majambazi

Gari la Polisi likiwa nje ya nyumba ya bwana Mtaki ambaye ameweka makazi ya muda eneo la shambani kwake Chapwa

Mkuu wa polisi Momba OCD -afande Chatanda akichukua maelezo ya nyongeza kutoka kwa majeruhi Mtaki  jana mchana alipomtembelea tena kwa mara ya sita tangu kutokea kwa tukio hilo. Kulingana na maelezo ya OCD Chatanda, maendeleo ya upelelezi yanaonyesha kuwa mazuri

Mguu ambao umechanwa na kuharibiwa na baruti pamoja na goroli za risasi

Mwandishi wa habari wa Uhuru na Mzalendo eneo la Mpakani (Tunduma na Mbozi) Bwana Shomi Mtaki akimwonyesha mmiliki wa Indaba blog jereha la risasi aliyopigwa October 11 usiku nyumbani kwake baada ya kuvamiwa na majambazi waliokuwa wakimtaka atoe fedha ati kwakuwa anamiliki Trekta lililokuwa limeegeshwa nje ya nyumba yake eneo la shambani kwake Chapwa