Waziri wa nishati na
Madini Mh Profesa Sospeter Mhongo jana ameruka viunzi sakata la kuvuja kwa mafuta ya diesel kwenye visima
vya maji katika mji wa Mlowo na kudai kuwa halihusiani na wizara yake
Akizungumza jana wakati akijibu swali la mmoja wa Madiwani
aliyetaka kujua serikali inafanya nini wakati wananchi wa Mlowo wakiwa afya zao
zikiwa hatarini kutokana na kuchota mafuta badala ya maji kwenye visima vya mji
huo.
Suala hilo
liliwasilishwa na diwani wa Myovizi Mh Cosmas Nzowa ambaye alihoji kama waziri
anayeshughulikia masuala ya nishati ambapo mafuta ya diseli ni sehemu ya
mamlaka ya waziri huyo ambapo waziri alikuwa akimkatiza katiza wakati diwani
huyo akiuliza
“masuala ya mafuta ya
diseli ninahusikaje mimi? Waulize NEMC hilo ni suala lao “ alisikika waziri
Mlongo kabla ya diwani huyo kufafanua
Diwani huyo alisisitiza
suala la Mafuta ni sehemu ya wizara ya Mlongo labda kama imebadilika na ndipo
Mlongo aliporuhusu aendelee kuuliza swali lake, “ haya endelea bwana” uliza tu
Hata hivyo pamoja na
swali hilo kuulizwa kwa lengo la kutaka
majibu yam h waziri, inaonekana waziri alilikwepa katika kutoa majibu pale ambapo alizungumzia zaidi masuala
ya Umeme na jitihada zinazofanyika
mkoani Mbeya na pia kwa wilaya ya mbozi
lakini kwenye mafuta ya Mlowo alikauka!
Kwa ujumla wakazi wa
mji wa Mlowo wamekuwa wakilalamikia hali mbaya ya maji ya visima vyao
kunakotokana na mwingiliano wa mafuta ya diseli yanayohofiwa kuvuja kutoka
kwenye bomba la Mafuta la TAZAMA ama kutoka kwenye moja ya visima vya mafuta
vilivyopo kwenye vituo vya Mlowo.
Diwani wa Myovizi Cosmas Nzowa akisalimiana na Mh Profesa Mhongo alipofanya ziara yake katika wilaya ya Mbozi kwa lengo la kukagua miradi inayotekelezwa na Wakala wa Umeme vijiji REA jana |
Katika majumuisho yake
kwenye kikao chake kilichofanyika ukumbi wa mkuu wa wilaya Mbozi, Waziri Mlongo
alielekeza wananchi kuwa na nia njema ya kugawa maendeleo sawia katika
meneo yote ya nchi badala ya kuwa na uroho wa kila fulsa kuwa kwenye maeneo
yao.
Hali hiyo
ilitokana na kila diwani aliyesimama
kwenye kikao hicho kuvutia umeme kwenye maeneo yake kuwa haujapitia, na ndipo
alipomwinua mbunge wa Mpanda –Katavi Saidi
Kessy na kumuuliza, hivi wewe Kessy kule kwako umepewa kiasi gani na REA?
Mh Kessy alijibu Bilion
10. Mheshimiwa waziri na Mkoa wa RUkwa
umepewa Bilion 30!
Ndipo alipodakia hapo
waziri na kueleza” Nyinyi Mbozi kama wilaya mmepewa Bilion 22.57 wakati wenzenu
Rukwa kama mkoa wamepewa Bilion 30 hamuoni kuwa mmepata kiasi kikubwa sana? Sasa
tukielekeza kila kitu kwenye wilaya yenu jamani tuwe na ulinganifu.