Adverts

Nov 1, 2013

MTOTO AWATOROKA WALINZI WA PAPA NA KUFANIKIWA KUMKUMBATIA PAPA NA KUFANYA VITUKO


 Mtoto huyu akiwa amemkumbatia papa baada ya kunyanyuka aakiwa amekaa na watoto wenzake eneo la jukwaa la papa kuhutubia
 Mtoto akifurahia baada ya kumkumbatia papa na kuonyesha vituko kwa staili ya mwendo wa mamiss
 Papa akikatuliza katotokwa kutoa baraka huku akimalizia ibada aliyokuwa akiiendesha
 Mtoto akiwa amekalia kiti cha papa baada ya kuridhika kupata baraka za papa

Na Indaba africa
MWISHONI  mwa wiki, katika hali isiyotarajiwa  Mtoto mdogo jasiri alinyanyuka na kwenda hadi alipokuwa amesimama  Papa Francis wakati alipokuwa akitoa hotuba na kumkubatia naye.

Mtoto huyu  alikuwa ni sehemu ya kundi la watoto ambao walialikwa kukaa karibu na Baba Mtakatifu wakati akiendesha misa ya wanafamilia  kutoka jamii mbalimbali eneo lake la kutolea Baraka la St Peters  Square .

Katika ibada hiyo iliyoambatana na mkutano wa Baraza la Kipapa  kwaajili ya kuombea familia lililofanyika  Vatican Oktoba 26. 

Kijana bila kujali ulinzi uliopo wala hofu alinyanyuka pale alipokaa na kwenda  upande wa Papa na kuwapita Makardinali hadi pale alipokuwa ameketi papa na kumkumbatia
 aidha mtoto huyo alianza kuonyesha vichekesho mbele ya papa na kuonyesha mithiri ya mwanamitindo baada ya kuridhika amemkumbatia papa hadi alipoketi na kukaa naye kwenye kiti chake


Baada ya kumwona mtoto huyu akiwa ameshika pindo mavazi yake, papa akiwa anaendelea na ibada alimkumbatia mtoto huyo na baadaye kuketi naye  huku watu wakishangaa hali hiyo.