Mar 23, 2014

JAMVI LA LIGI DARAJA LA KWANZA LAKUNJWA HUKU KIMONDO IKIRUKA KIMANGA KUSHUKA DARAJA

 
Na Danny Tweve
 
Timu ya Kimondo supersport club ya Mbozi mkoani Mbeya, imemaliza mzunguko wa pili wa ligi daraja la kwanza Tanzania kwa kuikamua Mlale JKT ya Songea bao 1-0 katika mchezo mkali uliochezwa uwanja wa CCM Vwawa.
 
Ulikuwa mchezo wa kasi na kusisimua tangu kuanza kwake, lakini kadiri dakika zilivyoyeya ndivyo mhemuko wa mashabiki kutaka goli la kuwahakikishia Kimondo kuendelea kucheza ligi daraja la kwanza ukizidi
 
Mchezo huo ulikuwa muhimu kwa Kimondo ili kujiweka katika mazingira ya kutoshuka daraja kutokana na Kimondo kuwa moja ya timu katika kundi hilo zilizokuwa na pointi 14 huku pia timu ya Mkamba ambayo ilikuwa mkiani ikiwa na pointi 13
 
Matokeo ya jana yanaifanya Kimondo ambayo ilikuwa kundi B kujipanga upya baada ya kutoa fulsa kwa timu ya Polisi Morogoro kuondoka ikiwa na ushindi kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Vwawa licha ya ukweli kwamba tayari Polisi moro ilikuwa imeshajitangazia kupanda daraja katika mchezo wake na Maji Maji Morogoro hivyo kufikisha pointi 28 ambazo zisingefikiwa na timu yoyote

Licha ya jitihada za wazi za kuvuruga mchezo huo zilizofanywa na MLALE JKT ikiwa ni pamoja na kocha wao kuamua kuzunguka uwanja mzima kinyume na taratibu za mchezo huku akikoromeana mara kwa mara na waamuzi, mchezo ulimalizika kwa Kimondo kunyanyuka ikiwa na ushindi wa bao 1-0


MBEYA CITY WATOKA NA NG'ARI NG'ARI MPYA ZA ZUKU TV

 Ng'ari ng'ari mpya za Timu ya Mbeya City kama zinavyoonekana pamba kali kwa rangi zao!!!

 

WIKI YA MAJI MAKETE- MKOANI NJOMBE YAADHIMISHWA KWA MAFANIKIO MAKUBWA


Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni mstaafu Aseri Msangi akipata maelekezo kwenye banda la idara ya maji kuhusu bili za maji, katika wiki ya maji kimkoa katika viwanja vya mabehewani Makete mjini.
Mkuu wa mkoa Kapt. Msangi akisikiliza maelekezo toka kwa mtaalamu wa maji, katikati ni mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro.
Mkuu wa mkoa akipata maelekezo kuhusu mfumo mzima wa maji Makete mjini unavyofanya kazi.
 Kikundi cha sanaa cha SUMASESU kikitumbuiza kwenye maadhimisho hayo ya wiki ya maji.
 Kikundi cha sanaa kijulikanachoa kama Mchana Hasarani kikikonga nyoyo za washiriki wa maadhimisho hayo.
 Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akizungumza kwenye maadhimisho ya wiki ya maji kimkoa katika viwanja vya mabehewani Makete mjini.
 Mkuu wa mkoa wa Njombe kapteni Mstaafu Aseri Msangi akihutubia wananchi waliofika kumsikiliza katika maadhimisho ya wiki ya maji kimkoa katika viwanja vya mabehewani makete mjini.
Mkuu wa mkoa akihutubia wananchi.Picha zote na Edwin Moshi, Makete

Mar 19, 2014

TUNDUMA MADEREVA WAFUNGA BARABARA, KISA DEREVA WA TANZANIA KUUMIZWA NA POLISI ZAMBIA

HABARI ZILIZOTUFIKIA MUDA HUU , NI KWAMBA SHUGHULI ZA MPAKA WA TUNDUMA NA ZAMBIA ZIMESIMAMA KWA MUDA BAADA YA ASKARI WA UHAMIAJI UPANDE WA ZAMBIA KUMJERUHI VIBAYA DEREVA WA ROLI LA UPANDE WA TANZANIA.
 
TUKIO HILO LIMETOKEA MAJIRA YA SAA 5.30 ASUBUHI BAADA YA DEREVA HUYO AKIWA ANAKAMILISHA TARATIBU ZA UHAMIAJI UPANDE WA NAKONDE, KULITOKEA UBISHANI KUDOGO ULIOPELEKEA KULAZIMIKA KUTOKA NJE ILI AWASILIANE NA TAJIRI WAKE KWA SIMU
 
KATIKA HALI YA MVUTANO HUO, NDIPO DEREVA HUYO ALIPOVAMIWA NA POLISI WA UPANDE WA ZAMBIA BAADA YA KUAMRIWA NA OFISA WA UHAMIAJI WA UPANDE WA ZAMBIA KUMKAMATA KWA KUHOFIA ALIKUWA AKIRIPOTI MAHALA MALALAMIKO YA NAMNA ALIVYOTENDEWA NA OFISA HUYO
 
DEREVA ALIDAIWA KUHUSISHWA NA MGOGORO HUO ALIKUWA NA ROLI LENYE NAMBA ZA USAJIRI T 131 AQU MALI YA KAMPUNI YA CITEX YA JIJINI DAR ES SALAAM
 
KATIKA KUHOJI SABABU ZA KUZUIWA KUZUNGUMZA NA SIMU, NDIPO ALIPOANZA KUCHUKUA KICHAPO CHA KITAKO CHA BUNDUKI MAENEO NYETI.
 
KONDA WAKE ALIVYOSHUHUDIA HALI HIYO ALIWATAARIFU MADEREVA WENZAKE NA NDIPO WALIPOAMUA KUFUNGA NJIA KWA MAGARI HATUA AMBAYO IMESABABISHA SHUGHULI ZA USAFIRISHAJI MPAKANI KUSITISHWA
 
SAA SABA KAMILI KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA UPANDE WA TANZANIA ENEO LA MPAKANI IMEINGIA UPANDE WA ZAMBIA KWA LENGO LA KUJADILIANA HALI HIYO KUPITIA UTARATIBU WA UJIRANI MWEMA AMBAO HUHUSISHA MAMLAKA ZA ENEO HILO.
 
 

Mar 18, 2014

NDEGE WA AJABU BUKOBA WAZIDI KULETA MAAFA, SASA YABAINIKA KUSABABISHA MAGONJWA YA NGOZI

Sakata la ndege wa ajabu katika kisiwa cha Musira mkoani Kagera wanaotoa kinyesi kinachodaiwa kuwa na sumu na kusababisha kuku na mbuzi kuteketea sasa taarifa za kitaalum zimedai kuwa  7% ya  watoto na 3% watu wazima wameathiriwa na kinyesi kutokana na kushindwa kupumua vyema.

  Hayo ni  sehemu ya matokeo ya dodoso la uchunguzi kuhusu ndege hao kwenye Manispaa ya Bukoba, ambapo afisa tarafa ABDON KHAWA ameitoa taarifa hiyo ya kitaalam mbele ya mkuu wa mkoa wa Kagera Fabian Masawe alipotembelea kisiwa hicho jana.


Bwana Kahawa amesema kuwa taarifa hiyo inaonesha asilimia 45% ya mapaa ya nyumba za mabati yamepata kutu na kutoboka kutokana na kinyesi cha ndege. Kulingana na taarifa hiyo asilimia 61% ya kuku na 6% ya mbuzi wamekufa kutokana na vinyesi.
Katibu Tarafa Bwana Kahawaakitoa taarifa kwa RC
Dokta Ruuta mganga mkuu wa mkoa wa Kagera
Mh Diwani kata Miembeni Richard Gasper Asilimia ya wakaazi wa Musira wanaupele na kuwashwa ngozi baada ya uvamizi wa ndege.
Mkuu wa mkoa na wataalamu pamoja na wanahabari wakishuka kwenye mtumbwi
Wakaazi wa Musira wakisikiliza ripoti ya wataalamu wa uchunguzi
Ni Wakaazi wanaugulia ngozi kutokana na kupata upele na ngozi kuwasha.
Hili ni kanisa la Orthodox kisiwani humo, ambalo limezungukwa na miti iliyojaa ndege hao Taarifa rasmi inasema 28% ya wakaazi wamekuwa na tatizo la kuumwa tumbo na kuharisha baada ya uvamizi wa ndege hawa.

Pia wakazi hawa asilimia 43% hawachemshi maji ya kunywa na 4% tu ya wakaazi wa Musira ndiyo wenye vyoo bora.

Hatahivyo sampuli zilizokusanywa na wataalamu kuanzia 11 mach adi 16 mach 2014, yamepelekwa kwa mkemia mkuu, ili kuchunguzwa kutokana na vitedea kazi hafifu katika kituo kilichopo mkoani Kagera, hivyo taarifa zimesubiriwa.
KUTOKA JAMII FORUMS

TANZANIA NA MALAWI ZATILIANA SAINI MKATABA WA ONE STOP BORDER POST

Uwekaji saini huo ulifanyika Lilongwe, Malawi siku ya Jumatatu tarehe 10 Machi, 2014 ambapo Waziri wa Fedha Mhe Saada Salum aliweza saini kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, wakati Waziri wa Biashara na Viwanda, Mhe. Sosten Gwengwe aliweka saini kwa niaba ya Serikali ya Malawi.
MALAWI1.JPG
Maafisa wa Tanzania na Malawi wakifanya maandalizi kabla ya Mawaziri kuwasili kwa ajili ya shughuli ya uwekaji saini Mkataba
MALAWI2.JPG

Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Salum (Mb), kushoto na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Malawi, Mhe. Sosten Gwengwe wakisaini Mkataba wa kuanzisha Kituo cha Pamoja cha Uhamiaji na Ushuru wa Forodha katika mpaka wa Songwe - Kasumulu. Hafla ya uwekaji saini imefanyika katika Ofisi ya Wizara ya Biashara na Viwanda, Lilongwe, Malawi tarehe 10 Machi, 2014.
MALAWI3.JPG
Mhe. Salum, kulia akitoa neno baada ya shughuli za kusaini Mkataba kukamilika. Anayemsikiliza ni Waziri wa Biashara na Viwanda wa Malawi, Mhe. Gwengwe.
(copy and paste from Mabadiliko forum)

KAMISHNA WA TACAIDS ASHTUSHWA NA ULEVI WA WANAOTUMIA ARV! ASEMA NI HATARI

Na Mwandishi wa Indaba Africa

Kamishna wa Tume ya kudhibiti UKIMWI TACAIDS Dk Violet Bakari  ametahadharisha uwezekano wa kutokea vifo zaidi na kutetereka kwa afya za watumiaji wa ARV ikiwa hawatapunguza  matumizi ya pombe.

Alisema ingawa kwa maeneo ya baridi baadhi ya watumiaji wa ARV wamekuwa wakisingizia hali ya baridi kuchangia unywaji wa pombe, amesema vivyo hivyo kwa maeneo ya joto pia imebainika watumiaji wa ARV wamekuwa watumiaji wa kileo hali ambayo amesema isitumike kama kisingizio cha kuhalalisha kuathiri afya zao.

 Akizungumza na vikundi na konga za watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI katika tarafa ya Igamba wilayani Mbozi, Kamishna huyo amesema, imebainika kuwa watu wanaotumia ARV wamekuwa watumiaji wakubwa wa pombe hasa vijiji, hali ambayo amesema kwa sehemu kubwa inachangiwa na kuimarika kwa afya zao hivyo kujiona wapo vizuri kama zamani.

Amesema uzoefu unaonyesha kadiri wanavyotumia dawa hizo na kuona afya zao zikiimarika, ndivyo wengi wao walivyojiingiza kwenye matumizi ya pombe hali ambayo amesema hawajatambua madhara yake kiafya na akawasihi afya zao zinazoimarika ziendane na uzalishaji kwaajili kujiweka vyema kiuchumi.

Alisema lengo la kuwawezesha kupata dawa hizo ni kuimarisha kinga zao na kuwawezesha kutumia fulsa ya afya bora katika kuendelea kutoa mchango wao kwa taifa na familia zao, tofauti na mtazamo wa wengi wao kuelekeza nguvu zao katika matumizi makubwa ya pombe

Kwa upande wake mkurugenzi wa tathmini na ufuatiliaji Dk Meshack Shimwela aliwataka wananchi kutochagua njia moja ya kukabiliana na maambukizi ya VVU na UKIMWI.

Akijibu maswali ya wananchi waliohoji muundo wa mipira ya kiume kutoziba sehemu kubwa ya maeneo ya siri na matokeo yake kusababisha maji maji kutoka kwa mtu mmoja kuhamia kwa mtu mwingine hivyo kuwepo hatari ya kuambukizana ikiwa mmoja atakuwa na majeraha katika mwili.

Dk Shimwela alisema, ni vyema wananchi wakatambua kuwa suala la matumizi ya kondomu za kiume linafanyika pale watumiaji wanapokubaliana na huku wakiwa timamu kiafya, lakini itakuwa maajabu kwa mtu kulazimisha kufanya mapenzi huku akitambua anavidonda mwilini hali ambayo hawezi kulifurahia tendo hilo.

“ni vyema tukatambua kuwa huduma tulizo nazo kila moja wapo hutumika kwa wakati, si vyema tukalazimisha kila jambo lifanyike na huduma moja” alifafanua Dk Shimwela

Katika ziara hiyo, tume imeridhishwa na utendaji wa afua za mapambano dhidi ya UKIMWI  ambapo watu wanaoishi na VVU wamekuwa na miradi ya kiuchumi hali ambayo inapunguza unyanyapaa na ubaguzi kwenye jamii wanazoishi. Takwimu za wilaya zinaonyesha kuna jumla ya wateja 11,500 walisajiliwa kutumia dawa za ARV katika wilaya ya Mbozi
MWISHO

 

CHIFU WA WANYIHA MWENE SHANTIWA MLOTWA AITAKA SERIKALI IWAACHIE MACHIFU KUADHIBU WAHALIBIFU WA MAZINGIRA


 Wajumbe waliohudhulia kwenye chanzo cha maji katika eneo la Halungu ambako mradi mkubwa wa maji utajengwa
 Mhandisi wa Maji Mbozi  Eckson Mwasyange akizungumza kwenye uwekaji jiwe la msingi
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi Erick Ambakisye akiweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji Halungu
 Chifu Mlotwa Shantiwa akipanda mti kwenye uzinduzi wa mradi wa maji Halungu
 Wakuu wa idara na wakazi wa Halungu wakipanda miti katika chanzo cha maji Halungu
 Mwandishi wa TBC Hosea Cheyo akiongozana na chifu Mlotwa Shantiwa
 Diwani wa kata ya Halungu Mh Simkoko akizungumza na wakazi wa kijiji hicho juu ya mradi wa maji unaotarajiwa kutekelezwa

Wazee wa kinyakyusa wakiingia kwa mbwembwe kwenye Ling'oma



na Mwandishi wa Indaba Africa-Mbozi

Mwenyekiti wa baraza la machifu wilayani Mbozi katika mkoa wa Mbeya Chifu Mlotwa Shantiwa ameitaka serikali kuachia baadhi ya mambo na hasa masuala ya adhabu kwamakosa ya  uhifadhi wa mazingira kwa mamlaka za kimila ili kuwezesha kujenga nidhamu katika jamii.

Akizungumza katika kijiji cha Halungu wilayani Mbozi, chifu huyo amesema sheria za kitaalam zimeonekana kushindwa kufanya kazi hasa kwenye uhifadhi wa vyanzo vya maji ambapo hali imeendelea kuwa mbaya licha ya sheria hizo kuwepo

Alisema ili kujenga nidhamu na kutia uoga katika jamii, ni vyema machifu wakaachiwa sehemu ya majukumu ya kuadhibu wanaoharibu mazingira ili kuwezesha vizazi vijavyo angalau kufaidi sehemu ya raslimali zilizopo

Aliyasema hayo wakati wa kuwekwa jiwe la msingi la mradi wa maji kwa vijiji vya Halungu na Sasenga vyenye zaidi ya wakazi 9,500, mradi ambao utagharimu jumla ya shilingi million 668 mpaka kukamilika kwake.

Mapema akizungumza na wananchi wa vijiji hivyo Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi  Erick Ambakisye  ameelezea kusikitishwa na ari ndogo ya uchangiaji asilimia 5% ya mradi ambapo katika kipindi cha miaka minne wananchi wamechangia shilingi million moja tu kati ya shilingi 32 milion walizopaswa kuchangia.

Alisema hali hiyo inaweza kukwamisha uwezekano wa fulsa zingine za miradi ya maendeleo kuelekezwa kwa wananchi hao.

Kulingana  na mhandisi wa maji wilaya ya Mbozi bwana Ackson Mwasyange, mradi  huo utaanza kutekelezwa mwezi April na unakusudiwa kukamilika mwezi March 2015, na kwamba ni miongoni mwa miradi mingine mitano inayotekelezwa wilayani Mbozi kwa kupitia program ya maji chini ya benki ya dunia.

Katika risala yao wananchi wa kijiji hicho wameonyesha kusikitishwa na ucheleweshaji wa mradi huo ambapo tangu mwaka 2004 serikali ilianzisha mchakato wa utekelezaji wa miradi hiyo mpaka sasa bado zimeendelea kutolewa taarifa za matumaini pasipo kupata huduma ya maji.

Mwisho

Mar 17, 2014

TACAIDS YAELEKEZA NGUVU MASHULENI

 Kamishna wa TACAIDS akiwa na ujumbe wake kufuatilia hali ya utekelezaji wa mipango ya elimu dhidi ya UKIMWI mashuleni