Oct 28, 2014
CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU CHA ZAMBIA CHAIJIA JUU TIMU YA WANAWAKE YA TAIFA
PRESS STATEMENT.
October 28, 2014
POSITION ON THE "SHEPOLOPOLO".
The Football Association of Zambia has noted with dismay the high level of indiscipline exhibited by the Senior Zambia National Women’s Soccer team after their elimination from the 2014 Africa Women’s Championships in Namibia.
This kind of behavior where a group of young ladies want to hold the Association to ransom is alien to football and cannot be tolerated and condoned.
Never in the recent past has the Association been made to fulfill so many international fixtures and tournaments as has been the case, the last two years, beginning with the qualification of the Under 17 women’s team to the Junior World Women’s Championships in Costa Rica. This was followed by the qualification of the Senior Women’s Team to their maiden Africa Women Championships in Namibia. And then came the qualification of the boys Under 17 and 20 teams to the Africa Youth Championships to be held in early 2015. This is besides the numerous local training camps for the local national team that are costing the Association dearly.
These fixtures and tournaments have taken a heavy toll on the Association’s finance base which has resulted in many sacrifices being made especially with regard to meeting costs for its various sub-committee meetings and other pertinent needs.
The Under 17 and 20 boys teams have both qualified to their respective 2015 African Youth Championship finals with little or nothing from the Association but pride and dedication to duty. The players from these two teams have not held the Association to ransom despite only getting their FIFA approved stipends from the Football Association of Zambia.
It must be further stated that the Association does not receive any form of financial assistance and support from the Government to fulfill programs both for the women and boys junior national teams. FAZ relies on the resources realized from sponsorships and gate revenue from International matches by the Senior National Team to meet these international fixtures.
It has been the resolve of the Association that neglecting junior and women’s programs will negate and impact negatively on the performance of the Senior National Team which is the torch bearer of Zambian football.
In must be emphasized that FAZ has sacrificed a lot of its time and resources to ensure that women and junior national programs are fulfilled, even to the extent of depleting the Association’s resources to the barest minimum.
There are so many players and officials who have sacrificed for this country who have never displayed this callous disregard for authority.
In this regard, The Football Association of Zambia will be taking steps to address issues of the women national football teams going forward.
George M Kasengele
GENERAL SECRETARY.
Oct 24, 2014
KOZI YA MAKOCHA YAANZA LEO
Release No. 164
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Oktoba 23, 2014
RAIS
WA TOC KUFUNGA KOZI YA MAKOCHA
Rais wa Kamati
ya Olimpiki Tanzania (TOC) Gulam Rashid kesho (Oktoba 24 mwaka huu) atafunga kozi
ya makocha ya Leseni C ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Hafla ya
ufungaji kozi hiyo iliyoshirikisha makocha 32 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar
na kuandaliwa na TOC kupitia Olympic Solidarity kwa ushirikiano na Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itafanyika saa 5 asubuhi kwenye hosteli za TFF
zilizopo Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Kozi hiyo ya
wiki mbili iliyoanza Oktoba 12 mwaka huu iliendeshwa na Mkufunzi wa Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) Ulric Mathiot kutoka Shelisheli.
Makocha
walioshiriki kozi hiyo ni Ahmed Suleiman Simba (Alliance), Akida Saidi (Lindi),
Ally Bushir Mahmoud (Zanzibar), Aloyce Akwilin (Pwani), Amin Rashid Mdowe
(Zanzibar), Augustino Dakto Damian (Katavi), Athuman Bilal (Shinyanga), Bakari
Shime (Tanga), Charles Mayaya (Shinyanga) na Choki Abeid (Geita).
Wengine ni Edna
Lema (Morogoro), George Melchior (Kagera), Godfrey Kapufi (Katavi), Hamis Mabo
(Kigoma), Hawa Bajangero (TWFA), Ibrahim Mulumba (Geita), Jemedari Said
(TAFCA), Kenny Mwaisabula (TAFCA), Madenge S. Omari (Mara), Milambo Camil
(Tabora) na Mohamed D (Ruvuma).
Pia wapo
Mohamed Ismail Laiser (Manyara), Mohamed Muya (Dodoma), Ngawina Ngawina
(Mtwara), Nicholas Kiondo (Ilala), Osuri Charles Kosuri (Simiyu), Rachel
Palangyo (TWFA), Salvatory Edward (Temeke), Seif Bausi Nassor (Zanzibar), Yusuf
Macho (Kigoma), Wilfred Mollel (Iringa) na Zacharia Mgambwa (Rukwa).
Makocha
watakaofaulu kozi hiyo watapewa Leseni C za CAF wakati watakaoshindwa watapewa
vyeti vya ushiriki tu.
IMETOLEWA NA
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Oct 20, 2014
HATIMAYE KIMONDO IMESALIMU AMRI MBELE YA TESSEMA, NI BAADA YA MCHEZO KURUDIWA
Na Mwandishi wetu,
Licha ya kupigana kiume, Kimondo imemaliza dakika 20 za kiporo cha mchezo wa jana ikiwa nyuma ya bao 1 lililofungwa jana wakati ikicheza na TESSEMA ya Manispaa Kinondoni.
Katika mchezo huo wa kumalizia dakika 20 uliochezwa kuanzia saa 4.30 asubuhi umemalizika kwa kosa kosa nyingi ambazo TESSEMA watakuwa wachoyo wa fadhira kama siyo kumshukuru kipa wa timu yao Hashimu Nzota ambaye ameokoa michomo mfululizo ipatayo mitano.
Licha ya Kimondo kubadili mchezo mara kwa mara katika dakika 20 ambapo walipiga kambi langoni mwa TESSEMA kwa takribani dakika 14 za mchezo, wakati wote mlinda mlango aliendelea kuwa kikwazo kutokana na uwezo wake kutokea mipira na kupangua majalo za umbali zilizoagiziwa kufuta matokeo ya jana.
Kwa matokeo hayo TESSEMA inaondoka mkoani ikiwa na pointi 3 za ugenini huku Kimondo ikianza safari za ugenini ikiwa na pointi 6 magoli 4 ya kufunga na 1 la kufungwa.
Licha ya kupigana kiume, Kimondo imemaliza dakika 20 za kiporo cha mchezo wa jana ikiwa nyuma ya bao 1 lililofungwa jana wakati ikicheza na TESSEMA ya Manispaa Kinondoni.
Katika mchezo huo wa kumalizia dakika 20 uliochezwa kuanzia saa 4.30 asubuhi umemalizika kwa kosa kosa nyingi ambazo TESSEMA watakuwa wachoyo wa fadhira kama siyo kumshukuru kipa wa timu yao Hashimu Nzota ambaye ameokoa michomo mfululizo ipatayo mitano.
Licha ya Kimondo kubadili mchezo mara kwa mara katika dakika 20 ambapo walipiga kambi langoni mwa TESSEMA kwa takribani dakika 14 za mchezo, wakati wote mlinda mlango aliendelea kuwa kikwazo kutokana na uwezo wake kutokea mipira na kupangua majalo za umbali zilizoagiziwa kufuta matokeo ya jana.
Kwa matokeo hayo TESSEMA inaondoka mkoani ikiwa na pointi 3 za ugenini huku Kimondo ikianza safari za ugenini ikiwa na pointi 6 magoli 4 ya kufunga na 1 la kufungwa.
Oct 19, 2014
MCHEZO WA KIMONDO NA KMC AMA TESSEMA WAVUNJIKA, NI BAADA YA UWANJA KUJAA MAJI
Kikosi cha TESSEMA au Kinondoni Municipal Council kilichoshuka dimbani uwanja wa CCM Vwawa |
Timu ya Kimondo ambayo marudio ya mchezo huo kesho wanapaswa kuyatumia vyema |
waamuzi wa mchezo huo wakiwa na team captains wa timu zote mbili |
Shabiki wa Kimondo akiogelea kwenye madimbwi ya uwanja huo baada ya mchezo kusimamishwa kutokana na maji kujaa |
Meza ya mwamuzi ikiwa inaelea kwenye maji |
Uwanja wa CCM Vwawa ukiwa umejaa maji |
Mwendo wa Madimbwi uwanjani |
Kamisaa wa mchezo huo Tinyendera akizungumza na viongozi wa timu zote kukubaliana kurejewa kwa mchezo huo hapo kesho majira ya saa nne asubuhi |
NA MWANDISHI WA INDABA AFRICA
Mchezo wa ligi daraja la kwanza baina ta TESSEMA na Kimondo uliofanyika uwanja wa Vwawa CCM Mbozi umevunjia dakika ya 74 baada ya mvua kubwa iliyoanza kunyesha dakika ya 55 kuharibu starehe ya mchezo kwa kujaza maji uwanjani
Mchezo huo umevunjika TESSEMA ikiwa mbele kwa bao moja lililofungwa na Moris Katumbo mnamo dakika ya 52 baada ya kumegewa pande zuri kutoka wingi ya kushoto lililosukumwa na Shabani Juma. Goli hili lilitokana na uzembe wa mmoja wa wachezaji wa Kimondo kuacha mpira akilalamikia mchezo mbaya uliofanywa na Ramadhan Choki, baada ya kona iliyopigwa na Mpoki Tauson wa Kimondo kuokolewa na walinzi wa TESSEMA.
Kosa hilo ambalo mwamuzi wa mchezo huo Hasan Abdalah hakuliona liliwagharimu Kimondo baada ya kupenyezwa mpira mbele na kumkuta Shaban Juma ambaye alichungulia na kumtupia mfungaji.
Kwa ujumla kosa kosa nyingi kwa upande wa Kimondo zingeweza kuzaa lulu ya mabao katika mchezo huo, hata hivyo TESSEMA watapaswa kuwapongeza walinzi wao ambao walikuwa vidume kukabili mashambulizi ya wenyeji.
Kulingana na taratibu za TFF kwenye kanuni za ligi hiyo mchezo huo utaendelezwa hapo kesho majira ya saa nne asubuhi kwakuwa dakika hazikuzidi 16.
Kanuni za TFF kwaajili ya ligi daraja la kwanza kifungu cha 3.(6) Kinaeleza kuwa " Iwapo mchezo ulishaanza na kuvunjika kwa sababu ya matukio ya dharura yasiyotarajiwa wala kusababishwa na timu husika, utapangwa kurudiwa kwa muda uliosalia, magoli yaliyofungwa na kadi zilizoonyeshwa katika mchezo huo zitaendelea kuhesabika".
Kwamazingira hayo Kesho kimondo inatakiwa kuyatumia mazingira hayo kuweka vyema rekodi yake ya uwanja wa nyumbani kwa kuhakikisha inapata mabao mawili katika kipindi cha dakika 15 ili kuondoa dosari ya bao moja walilolala nao jioni hii dhidi ya TESSEMA
Oct 15, 2014
ASHANTI MAJANGA" YAAMBULIA KICHAPO CHA 2 KAVU KUTOKA KIMONDO
Kikosi cha ASHANTI kilichoshuka dimbani dhidi ya Kimondo na kuambulia kichapo cha 2 Oclock |
Hii ndiyo sumu ya Ashanti al maarufu kama Kimondo KISSC iliyoshuka jioni ya leo na kutoka na ushindi wa mabao matakatifu 2-0 |
Benchi la Kimondo
Na Danny Tweve wa Indaba Africa,
Ikicheza uwanja wake
wa nyumbani Kimondo SSC ya Mbozi imeendelea kutunisha msuri kwa timu za maji ya
chumvi , mara hii kwa kuibatua Ashanti United
mabao 2-0 kwenye mchezo wa ligi
daraja la kwanza uliofanyika uwanja wa CCM Vwawa.
Hadi mapumziko , si
Kimondo wala Ashanti walikuwa wamechungulia nyavu za timu pinzani licha ya
Kimondo kukosa mabao matatu ya wazi katika gonga zilizochezwa kwenye lango la
ASHANTI lakini papara za wachezaji wake ziliiharibu mabao hayo.
Kipindi cha pili
kilianza kwa mabadiliko ya mfulizo yaliyofanywa na kocha wa timu ya Ashanti
ambayo yaliongeza uhai na mashambuzi, gonga na viminyo vya hapa na pale, hata
hivyo michezo ya kimjini mjini –zikiwemo rafu za hapa na pale, vipepsi na janja
janja ziliwagharimu Ashanti kwa
wachezaji wake wawili kupewa kadi za njano kwa kuwajeruhi wachezaji wa kimondo
ambao mmoja alishindwa kuendelea na mchezo.
Mnamo dakika ya 72
Kimondo kupitia kwa Michael Mwailusu
Bosco baada ya kutokea gonga nikugonge langoni mwa ASHANTI
kufuatia kona iliyopigwa na Mshaki Simbeye
Dakika ya 89 Kimondo
walitupia msumari wa moto langoni mwa Ashanti ulioenda moja kwa moja wavuni
bila mlindamlango kuuona mpira ulioanzia wingi ya kushoto , bao lililofungwa na
Geofrey Mwashuya ambaye katika mchezo huo alionekana wazi kuwa hatakuwa na timu
ya Kimondo kwenye dirisha dogo la usajiri kutokana na kiwango chake kuendelea kuvutia timu nyingi
za ligi kuu.
Ama kwa upande wa
mashabiki, burudani ya mchezo wa leo iliongezewa chachandu baada ya mashabiki
wa Mbeya City kukodi mabasi mawili kuja
kuipa sapoti Kimondo ya Mbozi hali ambayo iliufanya uwanja ulindime kwa shamra
shamra na mbwebwe za mashabiki hao.
Mchezo wa leo
uliochezeshwa na mwamuzi Kinugani kutoka Morogoro akisaidiwa na Alphaxad Mteta
kutoka Ruvuma, Cheyo kutoka songea , Kefa kayombo kutoka mbeya ulikuwa chini ya
kamisaa Zahra Mohamed mwamuzi wa siku
nyingi wa michezo ya kimataifa.
Oct 11, 2014
KIMONDO YAANZA KWA AMSHA AMSHA KAMA ZA MBEYA CITY, YAIBUTUA VILLA SQUARD 2 'OCLOCK!
Timu ya Kimondo katika mchezo wake na Villa Squard ikiwa kwenye ng'ari nga'ari mpya |
Timu ya Villa Squard katika pozi lapicha kabla ya mchezo huo |
KIMONDO SUPER SPORTS CLUB ya Mbozi imeanza vyema ligi daraja la kwanza kwa msimu wa pili tangu ipande daraja, kwa kuwainua mashabiki walifurika uwanja wa CCM Vwawa baada ya kuwanyunyizia mabao 2 kwa 0 timu ya Villa Squard ya jijini Dar
Ikiingia na Ng'aring'ari kali zinazoinyemelea Mbeya City, pamba kali za blue bahari moja makini sana, ilianza kuonyesha mazingira ya ushindi tangu dakika za mwanzo kutokana na mashambulizi ya mfululizo kuanzia dakika ya 35 hadi kipindi cha mapumziko ikiwa na bao moja mkononi
Bao la Kwanza kwa Kimondo lilipatikana mnamo dakika ya 41 kupitia kwa Geofrey Mlawa baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Geofrey Mwashuya ambaye alikuwa lulu kwa kuendesha mchakamchaka beki ya Villa muda wote
Dakika 45 za kipindi cha pili zilianza kwa kosa kosa nyingi zilizoiandama Kimondo baada ya kufanya mabadiliko kwa kumpumzisha Gofrey Mlawa ambaye alijeruhiwa dakika chache kabla ya mapumziko na nafasi yake kuchukuliwa na Dulla Jumanne, ambaye aling'ara kwa kuamsha mashambulizi ya mfululizo yaliyoipeleka Kimondo hatua ya kupata penati
Ilikuwa dakika ya 83 Geofrey Mwashuya aliihadaa ngome ya Villa kwa shuti lililomfikia Peter Methew ambaye akaunga msafara wa kwenda kumwona Kipa wa Villa Squard lakini kabla hajafanya mambo alivutwa jezi na mzee mzima Nurdin Bakari na hivyo mwamuzi kutoa penati kwa Kimondo ambayo ilifungwa na Mpoki Tauson ambaye aliihesabia Kimondo bao la pili dakika ya 85.
Baada ya bao hilo Villa waliamua kutembeza viatu mwanzo mwisho hali ambayo ilimfanya mwamuzi Salehe Mang'ola kutoka Dodoma kumzawadia kadi ya Njano Ramadhan Chombo Lidondo na mara kadhaa kujizuia kutoa kadi kutokana na makosa ya wazi wazi .
Dakika ya 88 Villa walifanya shambulio lililojengwa na mzee mzima Nurdin Bakari na kusababisha mmoja wa wacheza wa Kimondo kuunawa eneo la hatari na kusababisha penati ambayo hata hivyo mashabiki wa Villa wakiwa na matumaini ya kupoza mioyo kwa bao angalau 1, Mchezaji wao aliyevaa jezi 25 alipiga penati hiyo nje na kuufanya mchezo kumalizika Kimondo 2 Villa Squard 0