Adverts

Oct 20, 2014

HATIMAYE KIMONDO IMESALIMU AMRI MBELE YA TESSEMA, NI BAADA YA MCHEZO KURUDIWA

Na Mwandishi wetu,
Licha ya kupigana kiume, Kimondo imemaliza dakika 20 za kiporo cha mchezo wa jana ikiwa nyuma ya bao 1 lililofungwa jana  wakati ikicheza na TESSEMA ya Manispaa Kinondoni.

Katika mchezo huo wa kumalizia dakika 20 uliochezwa kuanzia saa 4.30 asubuhi umemalizika kwa kosa kosa nyingi ambazo TESSEMA watakuwa wachoyo wa fadhira kama siyo kumshukuru kipa wa timu yao  Hashimu Nzota ambaye ameokoa michomo mfululizo ipatayo mitano.

Licha ya Kimondo kubadili mchezo mara kwa mara katika dakika 20 ambapo walipiga kambi langoni mwa TESSEMA kwa takribani dakika 14 za mchezo, wakati wote mlinda mlango aliendelea kuwa kikwazo kutokana  na uwezo wake kutokea mipira na kupangua majalo za umbali zilizoagiziwa kufuta matokeo ya jana.

Kwa matokeo hayo TESSEMA inaondoka mkoani ikiwa na pointi 3 za ugenini huku Kimondo ikianza safari za ugenini ikiwa na pointi 6 magoli 4 ya kufunga na 1 la kufungwa.