Adverts

Nov 9, 2014

KIMONDO YAWAPIGISHA KWATA WAPIGANAJI WA MLALE JKT, YAWABANJUA 2-1 KWAOJKT MLALE HOII MBELE YA KIMONDO!!! YAAMBULIA TWO KWA MOJA!!!
Timu ya Kimondo SSC ya Mbozi imeendeleza ubabe tangu irejee nyanda za juu kusini baada ya kuibabua mabao 2-1 Timu ya Masoja ya Mlale Jkt katika uwanja wa majimaji Mjini Songea.

Ikicheza ugenini kwa kujiamini, Kimondo ilijikuta ainakubali kufungwa bao la mapema na kuwaamsha wenyeji Mlale JKT kwa kusherehekea dakika 30 za mwanzo

Kimondo iliamka kwa kasi na kuanza kupeleka mashambuzi kwenye lango la Mlale, ambapo mashambulizi hayo yalidumu kwa muda na kuwapatia bao la kusawazisha.
Kipindi cha Pili mchakamchaka wa Kimondo uliendelea na kuwawezesha kupata bao la pili na hadi mchezo unamalizika wenyeji wameondoka uwanjani wakiuguza maumivu ya kichapo kwenye uwanja wa nyumbani.
kwa mchezo wa leo Kimondo imefikisha pointi 11 ikiwa imeshinda michezo 4 na kufungwa 4 imeshinda magoli 10 na imefungwa mabao 8 ikipanda hadi nafasi ya nne kwenye kundi lao ambalo linaongozwa na timu za Majimaji na Friends Rangers zikifuatiwa na Lipuli na  Kurugenzi
Jumatano Kurugenzi itakuwa mgeni wa Kimondo kwenye uwanja wa CCM Vwawa kujiwinda katika michezo ya lala salama kabla duru la kwanza halijagonga ukingoni.