THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telegrams : "CABINET"
DAR ES SALAAM
Telephone : 2116898, 2116900/6
E-mail : chief@ikulu.go.tz
E-mail : ikulu@ikulu.go.tz
Fax : 2113425/2116914/2117272
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD
11400 DAR ES SALAAM.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa Makatibu
Wakuu wa Wizara kwa kuteua Makatibu Wakuu wanne wapya na kuhamisha
mmoja.
Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi na uhamisho wa Makatibu Tawala wa Mikoa.
Taarifa iliyotolewa mjini Dodoma jioni ya leo, Jumatano, Novemba 5,
2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa
walioteuliwa kuwa Makatibu Wakuu ni Dkt. Donan Mmbando ambaye anakuwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Yohana Budeba
ambaye anakuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi,
Mhandisi Mbogo Futakamba kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Dkt.
Adelhelm James Meru ambaye anakuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na
Maliasili.
Kabla ya uteuzi wake, Dkt Mmbando alikuwa Mganga Mkuu wa Serikali,
Dkt. Budeba alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Uvuvi na
Mifugo, Mhandisi Futakamba alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na
Dkt. Meru alikuwa Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Maeneo Maalum ya
Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA).
Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa Rais Kikwete amemhamisha Bibi
Maimuna Tarishi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kwenda kuwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria
Kuhusu uteuzi na uhamisho wa Makatibu Tawala wa Mikoa, Rais Kikwete
amemteua Bw. Charles Pallangyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi
wa Jamii kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Bw. Adoh Steven Mapunda,
Mkurugenzi Mtendaji, Manispaa ya Bukoba kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa
Arusha, Bw. Severine Kahitwa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita kuwa Katibu
Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro na Dkt. Faisal Issa, Katibu Tawala wa
Mkoa wa Kilimanjaro kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.
Wakati huo huo, Rais Kikwete amemteua Kanali (Mst) Joseph Simbakalia, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa EPZA.
Uteuzi huo unaanza leo na Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa
wataapishwa kesho, Alhamisi, Novemba 6, 2014, Ikulu, Dar es Salaam.
Mwisho.
Imetolewa na;Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
05 Novemba,2014