TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI - RELEASE NO. 111
TAREHE
03 JULAI 2015
STARS KUWAVAA THE CRANES KESHO
Taifa Stars inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premieum Lager
kesho jumamosi saa 10 kamili kwa saa za Afrika Mashariki itashuka dimba la Nakivubo
kucheza na wenyeji Uganda.(The Cranes).
Mecho hiyo ya kesho ni mchez wa marudiano kuwania kufuzu kwa
fainali za CHAN mwaka 2016 zitakazofanyika mapema mwezi Januari nchini Rwanda,
mgeni rasmi atakua Rais wa Uganda Yoweri Mseveni.
Kikosi cha Taifa Stars chini ya kocha wake mkuu Charles Mkwasa,
kiliwasili jijini Kampala jana usiku na kimefikia katika hoteli ya Grand Global
iliyopo jirani na chuo kikuu cha Uganda Makerere.
Taifa Stars imefanya mazoezi leo jioni katika uwanja wa Nakivubo
yakiwa ni mazoezi mepesi na mwisho kuzoea uwanja kabla ya mchezo wenyewe
utakaofnayika kesho jioni.
Kocha Mkwasa akiongelea kuelekea mchezo huo amesema, anashukuru
vijana wake wamefika salama wote, hali nzao ni nzuri, morali ni ya hali ya juu,
kikubwa wanatambua wana deni kubwa kwa watanzania hivyo kesho watapambana
kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.
Akiongelea hali ya hewa na mazingira ya timu ilipofikia, Mkwasa
amesema hali ya hewa ni ya kawaida baridi na mvua kidogo haina tofauti sana na
Tanzania, mazingira ya hoteli ni mazuri na kusema kikubwa kilichobaki ni kusaka
ushindi katika mchezo huo na vijana wake wapo tayari.
Wakati huo huo mashabiki zaidi ya 50 kutoka nchini Tanzania
wanatarajiwa kuwasili kesho jumamosi alfajiri wakitokea jijini Dar es salaam kuungana
na watanzania wengine waishio nchini Uganda kuishangilia timu ya Tanzania
itakapokuwa ikipimbana na Uganda katika uwanja wa Nakivubo.
Mawasiliano ya Afisa Habari wa TFF aliyepo Uganda ni +256 780 177008
NB: picha za mazoezi ya Taifa Stars Nakivubo leo zimeambatanishwa
IMETOLEWA
NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)