Adverts

Apr 7, 2009

JAMANI KUOA KUZURI

Huyu ni mdau wangu wa karibu, siku hii nadhani hatakuja kuisahau manake ndiyo aliingia kwenye ukurasa mwingine wa maisha, nawatakia maisha mema wote walioingia na kupitia hatua hii

UJUMBE UMEFIKA

Bango likionyesha kuwa wanawake hawabeep!!!! hii ilikuwa moja ya harakati za wanawake wilayani Mbozi kujieleza mbele ya jamii katika maadhimisho ya siku ya wanawake- iliyofanyika huko ITAKA.

ADP MBOZI nao wamo

Mh Diwani Sinjela wa mjini Vwawa akikabidhi msaada wa sare za mwanafunzi kwa mmoja wa walezi wa watoto wanaoishi katika mazingira magumu Vwawa. Msaada huu ulitolewa na shirika la ADP Mbozi moja ya mashirika yenye mchango mkubwa katika maendeleo ya wilaya ya Mbozi. Bravo ADP Mbozi

Masuala ya Maendeleo vijijini

Hii ni timu ya watoto wa Mzee Darajas, yaani Babu yangu, hapa yupo baba mzazi mzee Nzilani Awdst Tweve yeye anazungumza zaidi Kizulu si unajua mambo ya kufanya kazi migodini kule uzuluni? Siyabonga Nkosi!!

CHIFU NAYE YUMO KUPAMBANA NA UJINGA

Hii ni timu ya Mila na desturi iliyomkaribisha JK alipotembelea wilaya ya Mbozi, alivishwa pamba za kimila kumtambua kama "mwene" mzee huyu kutoka kijiji cha Hatelele anasisitiza kuwa pamoja na kupewa uchifu, jukumu kubwa ni kuhakikisha watoto wa Mbozi wanakwenda shule!

Jengo la kitegauchumi la NSSF Mbozi

Huu mjengo ndiyo sura ya Mbozi, tunawashukuru NSSF kwa kutambua umuhimu wa kuipa tafu Mbozi kwa kujenga jengo lenye kuleta sura nzuri, hapa bwana ndilo ghorofa lililopo barabarani unapoelekea Zambia!! Mbozi tumo.

KAMERA NAZO ZIPO BWANA

Waala huu sio mzigo ni tukamera tuchache, tena zinginenimeziacha nyumbani jumla ninazo arobaini na tisa!!!! ndivyo anavyonekana huyu mpiga picha akiwa na mzigo wa kamera kumvizia JK angalau apate ya ukumbusho!!! pembeni ni mpiga picha wa JK aliyepatikana jina moja la Lukuvi akiwa anamshangaa jamaa!!!! hii yote matunda ya amani ingekuwa nchi zingine haruhusiwi kusogea na vikamera vyake !!!!!!

Mbozi Nzuri bwana hata Jk ameipenda

Rais Jakaya Mrisho Kikwete siku alipotembelea wilaya ya Mbozi, kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji CRDB Bank Dr Charles Kimei, akifuatiwa na Mama Salma Kikwete. Wengine ni watumishi wa benki ya CRDB, hii ilikuwa ni tukio la uzinduzi wa tawi la CRDB mbozi

Jioni Mbozi huwa hiviiii

Hii yote ni madhari ya kuvutia katika wilaya ya MBOZI, jua linaelekea kuzama, lakini ni kwa kiasi gani tumetumia fulsa za utalii kuitangaza wilaya yetu? Karibuni Mbozi, nchi yenye neema na utajiri wa vivutio.

Danny

Timu ya veteran Simba katika mji wa Vwawa

Timu ya Veteran Mjini Vwawa katika Wilaya ya Mbozi ,imekuwa na utaratibu wa kuwafanyia mauaji ya mwaka kila mara inapokutana na wapinzani wao Veteran Yanga. Mechi ya hivi karibuni itafanyika wakati wa siku kuu za pasaka. Subiri Matokeo.
Danny