Adverts

Apr 7, 2009

Mbozi sasa macho kwenye elimu

HALMASHAURI YA WILAYA YA MBOZI (Barua zote ziandikwe kwa Mkurugenzi Mtendaji) Simu Na. 025 - 2580272 P.O. Box 3, Fax Na. 025 – 2580278 Mbozi – Tanzania E- Mail mbozi@iwayafrica.com Wilaya ya Mbozi imekiri kunufaika na utekelezaji wa mradi wa maendeleo ya Jamii TASAF kutokana na mchango wake katika maendeleo ya sekta ya elimu. Kiasi cha shilingi million 412,664,558.00 zimeelekezwa kwenye utekelezaji wa miradi ya Ujenzi wa mabweni, Nyumba za walimu, na madarasa katika vijiji 25 vya wilaya ya Mbozi. Akizungumza na balaza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Mbozi, Mkuu wa wilaya ya Mbozi amesema moja ya mambo ya kujivunia ni hatua ya kuongezeka kwa shule za sekondari kutoka 12 wakati akiingia wilayani Mbozi hadi kufikia shule 52 sasa. Anaeleza kuwa hatua hiyo kwa sehemu kubwa inatokana na wananchi kudhamilia katika kujikomboa na ujinga kulikochangiwa na kuungwa mkono na miradi ya Maendeleo kama TASAF na mipango mingine. Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi bwana Levison Chilewa anaesema mafanikio hayo ni sehemu ya mikakati iliyowekwa na watendaji wa halmashauri ya wilaya kwa ushirikiano na madiwani wao kuhakikisha kuwa angalau watoto wanaohitimu darasa la saba na kufaulu kwenda sekondari wanapata nafasi. Kwa mwaka 2009/2010 halmashauri ya wilaya ya Mbozi inakusudia kukamilisha ujenzi wa mabweni 13 katika shule za sekondari za kata kupitia fedha za Mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF na nguvu za wananchi. Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi bwana Aden Mwakyonde anasema ukombozi wa wananchi utatokana na elimu kwakuwa maeneo mengine kama uwezo wa kipato tayari yameshaonyesha mafanikio kutokana na pato la zao la kahawa ikilinganishwa na wilaya zingine za mikoa ya nyanda za juu kusini. Ni ukweli usiopingika kuwa wilaya ya Mbozi imekuwa na utajiri wa fedha miongoni mwa nwananchi wake unaochangiwa na kipato kikubwa cha zao la kahawa ,lakini bado wananchi wake wamekuwa wakiishi maisha ya ujima kutokana na mfululizo wa matukio ya kinyama yanayoripotiwa na vyombo vya habari yakiwemo mauaji ya uchunaji ngozi. Hali hii inadhihirisha kuwa bado suala ya elimu lipo nyuma na ndiyo sababu wilaya imeweka suala la elimu kama kipaumbele chake katika kuwezesha mazingira ya kusomea yanaimarishwa na shule kuwa eneo la kuvutia watoto kuikimbilia elimu badala ya kuikimbia elimu. Takwimu za ubora wa majengo zinaonyesha kuwa wilaya ya Mbozi ni miongoni mwa wilaya nchini zinazoongoza kwa kuwa na shule bora za msingi (majengo) ambapo wastani wa halmashauri za wilaya, manispaa na miji 15 hutembelea kwa mwaka kujifunza na kuona ujenzi huo. Katika kufanikisha jitihada hizo wilaya ya Mbozi imeanza harakati za kupanua mfuko wa elimu ambapo inakusudia kukusanya kiasi cha shilingi Bilion 12 kwa awamu tatu, awamu ya kwanza ikilenga kukusanya kiasi cha shilingi billion 3 kwa mwaka. Wanananchi wanaeleza kuwa kuimarishwa kwa miundombinu hasa barabara zinazofika vijijijini mwao ni mwanzo mzuri wa kufanikisha mpango wa kuinua elimu vijijini mwao kwasababu sasa watoto wataweza kwenda na kurudi kwenye shule za kata tofauti na mazingira ya awali. Kiasi cha shilingi Bilion 1.4 zilizoelekezwa na mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF wilayani Mbozi zinakusudia kuchangia mabadiliko makubwa ya ukuaji kiuchumi kwakuwa sehemu kubwa ya fedha hizo zimeelekezwa katika maeneo chochezi ya uchumi ingawa yapo katika huduma za jamii anaeleza afisa mipango bwana Nyarubamba. Chini ya mpango huo barabara 8 na madaraja matano vimejengwa kwa kiasi cha shilingi million 428 kiwango ambacho anaeleza kuwa ni mrija muhimu katika kuchavusha uchumi wa wilaya ya Mbozi hasa katika kupeleka pembejeo wakati wa uzalishaji na kusafirisha mazao baada ya kuvunwa tayari kwenda sokoni. Mkuu wa wilaya anayemaliza muda wake Bi Halima Kihemba anasema kuwa moja ya maeneo ambayo bado yanahitaji msukumo wa pekee ni vita dhidi ya matukio ya ushirikina ambayo yameiweka wilaya kwenye sura ya ujima. Anasema kura za maoni juu ya watu wanaojihusisha na vitendo vya kishirikina, mauaji ya albino na wizi na uuzaji wa dawa za kulevya ni viashiria dhahiri kuwa wananchi wamechoshwa na matukio hayo ni kwamba takwimu za waliopigiwa kura zinaonyesha majina mengi kujirudia rudia dalili zinazoonyesha kuwa wananchi wanataarifa zitakazosaidia kazi ya kuwachunguza watuhumiwa hao. Hata hivyo yapo maeneo yanayohitaji zaidi msukumo hasa matumizi ya utajiri uliopo mara baada ya kwisha kwa msimu wa kuuza kahawa yao, wengi wa wakulima wanaelekeza kwenye matumizi yanayochochea migogoro miongoni mwao. Mfano ni ongezeko la kesi za ugoni kila mara baada ya msimu wa kuuza kahawa, hii inadhihirisha kuwa sehemu kubwa ya mapato hayo hutumika katika masuala yasiyo changia tija na maendeleo moja kwa moja. haya yote yanabaki kuwa ni sehemu ya changamoto za mafanikio yaliyopo,lakini kubwa zaidi ni wananchi kutambua fulsa zilizopo katika kujiletea maendeleo kwa wao kupokea program za elimu zinazohamasishwa sasa ili waweze kupiga hatua kama ilivyo kwa mikoa mingine kama Kilimanjaro. Kuwepo kwa mpaka wa Tunduma iwe fulsa nyingine kwa wananchi wa mbozi kujifunza ustaarabu wa maendeleo kwa pande zingine kama Zambia, DRC kongo nk, haya yote yanazidi kupanua fulsa za kukimbia kimaendeleo wakati wilaya zingine zikienda mwendo wa kinyonga. Dhamira ipo na wananchi wanania, chamsingi ni kusimamia dhima na moto wa wilaya ya Mbozi wa Mbozi maendeleo, maendeleo yataletwa na sisi wenyewe kwa ushindani!!!!!!!!!!!!!! Danny Tweve