Apr 3, 2009
WACHINA WAKABIDHI MAJENGO YAO
Kampuni ya ujenzi barabara na Madaraja ya China imekabidhi majengo yake manne yenye thamani ya shilingi million 33 ili yatumike kwaajili ya makazi ya walimu sita wa shule ya sekondari Ihanda katika wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.
Majengo hayo ni sehemu ya raslimali za kampuni hiyo baada ya kuvunja kambi yake ya ujenzi wa barabara ya Songwe hadi Tunduma hivyo kuombwa na serikali ya wilaya kuyaachia majengo hayo ili yaweze kutumika kama makazi ya walimu.
wa kwa mradi wa barabra mwaka 2005.ambikabidhiano hayo yaliyofanywa kati ya mwakilishi wa kampuni hiyo Luteni Mstaafu Michael Esanju na Mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya Mbozi bwana Leornard Magacha na Mkurugenzi wa wilaya Bwana Levision Chilewa pia yamehudhuliwa na wanafunzi wa shule hiyo ambao wameyapokea kwa shangwe.
Wakizungumzia hatua hiyo Mwakilishi wa mkuu wa wilaya Bwana Leonard Magacha, Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya bwana Levison Chilewa na baadhi ya wanafunzi wamesema hatua hiyo inakwenda sambamba na mkakati wa wilaya wa kuboresha mazingira ya kusomea na kufundishia na kwa upande wa halmashauri itahakikisha majengo hayo yanakarabatiwa kukidhi ubora
Kwa upande wake afisa elimu wa wilaya ya Mbozi bwana Juma Kitabuge na mwakilishi wa kampuni ya China Road and Bridge Cooperation Luteni mstaafu Michael Esanju wamesema msaada huo unaifanya kampuni kuwa sehemu ya mafanikio yatakayofiwa katika siku za baadaye katika kuandaa vijana walioelimika kutoka kwenye kata ya Ihanda
Danny