Adverts

Sep 26, 2010

WAANDISHI WAPATA AJALI IRINGA

Na Danny Tweve, Mbeya. Mwenyekiti wa chama cha wandishi wa habari mkoa wa Mbeya NICO MWAIBALE na katibu wake Mkuu Bwana Patrick Kosima wamenusurika kufa katika ajali ya gari iliyotokea leo mchana katika msitu mkuu wa Sao hill Mafinga. Wakisafiria gari aina ya Suzuki Escudo V6 wandishi hao walioambatana na mkewe Nico Mwaibale Bi Laura Njau gari lao lilipasuka gurudumu la mbele na kupinduka mara nne hadi korongoni. Hata hivyo kwa kudra za mwenyezi mungu wote wamenusurika ingawa wana majeraha katika maeneo mbalimbali ya mwili. Inaelezwa na mwaibale kuwa ajali hiyo imetokea wakati akielekea jijini Dar es salaam kujiandaa kwaajili ya kuhamia mkoa wa Tabora ambako amehamishiwa kwenda kuimarisha Timu ya TBC mikoani. Akiwa kwenye eneo hilo inadaiwa gurudumu la mbele lilipasuka na kubiringika mara tatu hadi kwenye korongo ambapo kutokana na msaada wa mikanda waliyokuwa wamejifunga, hawakuweza kupata majeraha makubwa ingawa walibanwa na mikanda mpaka walipookolewa na raia wema. Nico amepongeza ushirikiano uliopatikana kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Mfindi Bi Darrly Rwegasira ambaye alipopigiwa simu na wandishi hao aliagiza haraka mganga mkuu wa wilaya pamoja na polisi kutoa gari la wagonjwa na kuweka ulinzi wa kutosha katika eneo la tukio hivyo kupunguza uwezekano wa wizi ingawa wananchi wa eneo hilo walitoa ushirikiano wa kutosha kabla ya msaada wa polisi. Majeruhi wote walikuwa bado wanaendelea na matibabu katika hospitali ya wilaya Mafinga.