Adverts

Jan 19, 2011

Dkt. Nchimbi akutana na wamiliki wa vyombo vya habari nchini

Dkt. Nchimbi akutana na wamiliki wa vyombo vya habari nchini: "

Mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari nchini Reginald Mengi (kulia) akiongea jambo wakati wa mazungumzo baina yao, viongozi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) na waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo. Anayemsikiliza ni Waziri wa Habari, vijana, utamaduni na michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi

Mkurugenzi Msaidizi kutoka idara ya Habari (Maelezo) Raphael Hokororo akifafanua jambo kuhusiana na sera ya habari wakati wa mazungumzo baina ya wamiliki wa vyombo vya habari nchini (MOAT), viongozi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Waziri wa Habari, vijana, utamaduni na michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga akimkabidhi moja ya vitabu vilivyotengenezwa na baraza hilo Waziri wa Habari, vijana, utamaduni na michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi (kulia ). Wamiliki wa vyombo vya habari nchini (MOAT) na viongozi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) walikuwa na mazungumzo ya kujadili mambo mbalimbali kuhusiana na taaluma ya habari na waziri Dkt. Nchimbi leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.

Waziri wa Habari, vijana, utamaduni na michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi (wa n ne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wamiliki wa vyombo vya habari nchini (MOAT) na viongozi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) mara baada ya kumalizika kwa mkutano wao ulioganyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.

"