Adverts

Jan 21, 2011

JK azindua uchangiaji wa kituo cha wanafunzi UDSM, akutana na mkurugenzi mkuu wa Commonwealth council na ujumbe wake

JK azindua uchangiaji wa kituo cha wanafunzi UDSM, akutana na mkurugenzi mkuu wa Commonwealth council na ujumbe wake: "
JK akimkaribisha Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Waziri mkuu Mstaafu Joseph Sinde Warioba wakati wa hafla ya kuchangia ujenzi wa kituo cha Wanafunzi uliofanyika ikulu jijini Dare s salaam usiku kuamkia leo.Katikati ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandala.Zaidi ya shilingi Bilioni 1.6 zilikusanywa katika hafla hiyo ya uzinduzi ambapo Rais Dr.Jakaya kikwete alichangi jumla ya Shilingi milioni kumi.
JK akipokea mchango wa Shilingi elfu kumi kutoka kwa mpigapicha wa gazeti la Jamboleo Richard Mwaikenda wakati wa hafla ya uzinduzi wa kuchangia ujenzi wa kituo cha wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
JK akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi mkuu wa Commonwealth Council Dr.Mohan Kaul(kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Bwana Reginald Mengi(kulia) mara baaada ya kufanya mazungumzo na Dr.Mohan pamoja na ujumbe wake ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.Wengine katika picha ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwezeshaji na Uwekezaji Dr.Mary Nagu(wapili kushoto), Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Juma Mwapachu(wanne kushoto) na kulia Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Emmanuel Ole Naiko. Picha zote na mdau Freddy Maro wa Ikulu.
"