Adverts

Jan 19, 2011

KEYSHIA COLE AMFUKUZA KAZI MENEJA WAKE

KEYSHIA COLE AMFUKUZA KAZI MENEJA WAKE: "

Hivi karibuni alifyatua album iliyokwenda kwa jina “Calling All Hearts“.Katika hali ambayo hakuitegemea,mauzo ya album hiyo hayakuwa mazuri ingawa katika charts za Billboards ilipanda mpaka kufikia # 9, hiyo haikumridhisha Keyshia Cole.

Afanyeje? Mwenyewe anasema kupitia Twitter kwamba “Endapo watu waliokuzunguka hawabadiliki,unachotakiwa ni kuwabadilisha watu waliokuzunguka”

Akaongezea na kusema kwamba “Kuanzia sasa Manny Halley hayupo tena katika menejimenti”.Hiyo ni njia rahisi tu ya kuiga msemo wa Donald Trump wa “You are Fired”

Wengi mnaweza kumkumbuka Manny Halley kutoka katika Reality Show ya Keyshia Cole iliyokuwa inarushwa kupitia BET ya “The Way It Is”.Ni yule jamaa ambaye alikuwa na Keyshia Cole kila sehemu akifanya kazi zake kama Meneja na pia kusuluhisha hata mambo ya familia yaliyokuwa yakimwandama Keyshia Cole. Ni muda wa mabadiliko.Lets see how this change will help Keyshia.

"