Adverts

Jan 15, 2011

KISWAHILI LUGHA ISIYOJIKUNYATA; ISIYOLALA …

KISWAHILI LUGHA ISIYOJIKUNYATA; ISIYOLALA …: "

Mtangazaji Charles Hillary wa BBC Swahili, akimhoji mgeni rasmi wa mkutano wa Diaspora, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Maendeleo ya Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe (picha na Baraka Baraka wa Urban Pulse, Reading).

Baadhi ya Wabongo nyumbani wamelalamika kwamba kongamano la Watanzania Uingereza (London Diaspora Conference) wikiendi iliyopita halikuwa na maana yeyote.

Labda upo kweli; labda si kweli.

Maelfu ya wataalamu wanaishia nchi za nje huku ujuzi wao ukihitajika sana nyumbani. Akili zao zinaishia chini; lakini si kwamba hawaijali Bongo baba. Madhumuni ya kongamano hili la London yalikuwa kuangalia mustakabal wa wananchi hawa. Jamii yetu changa inahitaji utaalamu wao.

Tuyaache hayo, kwanza.

Moja ya mada iliyowasha sana sigara, ilikuwa suala la Mtanzania na pasi mbili (“dual passport” au “dual citizenship”).

Wakti mkutano huu mahsusi ukiendelea baadhi ya wazungumzaji waishio huku Uzunguni walisikika wakisema : “Uraia Mbili” ama “ Uraia Miwili” (du!!!), “Citizenship mara mbili”, na “Uraia mara mbili”….. lakini….

URAIA PACHA, ilikuwa kiboko.

URAIA PACHA….!!!

Aliyestawisha nahau au msemo huu si mwingine bali mtangazaji wa Kiswahili, Idhaa ya BBC, Charles Hillary, ambaye pia aliteuliwa kama mchangamshaji (MC) wa makutano. Na katika wadhifa huo mboreshaji huyo wa Kiswahili Mama (Kiswahili Babu) akasaidia kutangaza neno jipya la Kiswahili fasaha linalomaanisha: MTU MWENYE URAIA WA NCHI MBILI.

Kiswahili ni lugha inayokua; isiyolala; lugha askari; inayoruka; yenye mabawa : mbayuwayu, yange yange; duma mwenda mbio; jogoo asiyechoka kuwika; vigelegele; lugha moto ya Waafrika.

Hongera kaka Charles Hillary!!!!!

" new post