Adverts

Jan 21, 2011

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI KENYA AFAGILIA BONGO

Na Danny Tweve

Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka jiji la Mombasa Anastazia Mkabwa ambaye hivi karibuni ametamba na kituchake cha KIATU KIVUE" amekiri kuwa Bongo ni nuksi kwa vipaji vya Uimbaji wa Gospel na masauti kwa ujumla hata kwenye miziki ya kimatiafa(isiyo ya dini).
Akizungumza asubuhi hii kwenye kipindi cha cha Sanii na Sanaa (DAMKA) cha Luninga ya  KBC Bi Anastazia Mkabwa amesema tangu kibao hicho amshirikishe Rose Mhando, ameona kabisa upako wa wabongo kwenye uimbaji na kwamba albamu inauza balaa.
Akihojiwa na mwendeshaji kipindi hicho bi Robi alitaka kujua kwa ujumla mziki wa Gospel wa Bongo na wanamziki wake kwa ujumla ukilinganisha na Kenya nani wakali, na mziki gani unapendwa kati ya nchi hizo mbili alikiri wazi kuwa Tanzania wana vipaji sana hata mziki wake wa kimataifa haulingani kabisa na Kenya, kila wimbo wa Tanzania unahit!

Alisema baada ya kukutana na Rose mhando walitaniana sana baada ya Rose kumwona mwimbaji huyo wamefanana na akamuuliza labda baba yangu alichepuka nje kidogo akaja huko kwenu ndiyo ukazaliwa wewe manake tunafanana "
Anaeleza kuwa katika albamu yake yenye nyimbo 10 kati yake nne amemshikrikisha Rose Mhando na kwamba bado anakusudia kuendelea kushirikiana na Watanzania.
kuhusu wimbo huo wa Kiatu Kivue unaoonekana na mipasho kiaina amesema umekubalika sana Mombasa ambako ni pwani hasa kwa staili yake ya mipasho ambao unazungumzia wanawake kuzengea waume za watu, na kwamba licha ya kundi kubwa katika eneo la Mombasa kuwa waislamu wimbo wake umekuwa ukipendwa na makundi yote na akaeleza kuwa kwake anaona baraka kubwa.
Akizungumzia mipango yake ya hivi karibuni amesema yupo kwenye hatua za kujenga studio yake eneo la Mombasa ambako anataka kupunguza usumbufu wa wasanii wa Mombasa kwenda kurekodia nyimbo zao Tanzania ama Nairobi na kwamba inatarajiwa kukamilika mwezi June, 2011.
Baadhi ya nyimbo alizoshirikiana na Rose Mhando ni pamoja na Wanakudharau, Mungu atukuzwe, Tabu zangu zitakwisha na Kiatu Kivue ambao kila kituo cha redio hasa FM za dini vimekuwa vikikikung'uta ile mbaya!.