Nahodha wa timu ya mpira wa pete ya Mkoa wa Morogoro akilinyanyua juu kombe la ubingwa wa UMITASHUMTA. Moro waliifunga timu ya Mkoa wa Mbeya kwa magoli 24 kwa 16 katika mechi ya fainali.
Washindi wa pili. Nahodha wa timu ya soka ya Mkoa wa Morogoro, Hosten Francis akipokea zawadi ya kombe kutoka kwa Mgeni rasmi naibu Waziri wa Elimu Mheshimiwa Philip Mulugo.
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Elimu Mheshimiwa Philip Mulugo katikati, shoto ni Naibu Katibu Mkuu OWM TAMISEMI anayeshughulikia Elimu bwana Jumanne Abdallah Sagini na kulia ni Naibu Waziri wa Nchi OWM TAMISEMI anayeshughulikia elimu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa. Serikali kupitia OWM-TAMISEMI ilifanya uamuzi wa kuyarejesha mashindano haya baada ya kutofanyika kwa miaka 10 mfululizo.
Wanamichezo kutoka Mkoa wa Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja na vikombe vyao mwishoni mwa mashindano ya UMITASHUMTA ambayo yalimalizika kwa mafanikio katika viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha.
Nahodha wa timu ya soka kutoka Mkoa wa Mbeya Yona Mtulo akilibusu kombe la ubingwa wa UMITASHUMTA mara baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi Naibu waziri wa Elimu Philip Mulugo. Katika Mchezo wa fainali, Mbeya waliifunga Morogoro kwa magoli 4 kwa 1.
> Mchezaji mpira wa pete wa mkoa wa Dar es salaam Mariam Yusuf ambaye aliibuka kuwa mchezaji bora kwa upande wa mpira wa pete akisalimiana na mgeni rasmi Naibu Waziri wa Elimu Mheshimiwa Philip Mulugo kabla ya kumkabidhi zawadi yake.
Wachezaji wa Mpira wa miguu kwa upande wa watoto wenye mahitaji maalum kutoka Mkoa wa Dar es salaam nao waliibuka washindi katika michuano hiyo wakifurahia zawadi yao ya kikombe walichokabidhiwa na mgeni rasmi.
Mchezaji bora wa michuano ya UMITASHUMTA kwa upande wa mpira wa Miguu Hosten Francis kutoka Mkoa wa Morogoro akipozi na zawadi yake mbele ya Mgeni rasmi Mheshimiwa Philip Mulugo. Kijana huyu alikuwa kivutio cha kipekee kwenye mashindano ya mwaka huu ya UMITASHUMTA kwa kusakata kandanda safi ambayo iliwaacha midomo wazi mashabiki wengi
walioshuhudia michuano hiyo
"