Jan 25, 2011
Omar al Bashir Akubali Matokeo Ya Awali
Omar al Bashir Akubali Matokeo Ya Awali: "
Rais Omar al Bashiri wa Sudan
Rais wa Sudan, Omar al Bashir, amesema amekubali matokeo ya awali yanayoonyesha wapiga kura Kusini mwa nchi hiyo, wameamua kwa kauli moja kujitenga na Sudan ya kaskazini katika kura ya maoni iliyopigwa kati ya 9 na 15 mwezi huu.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara kwenye mji wa Kaskazini wa Al-Damir, jimbo la Mto Nile, Rais Bashir amekiri kuwa raia wa kusini wameamua kwa asilimia 99 kujitenga.
Al Bashir aliwataja wale wanaotarajia kunaweza kutokea maasi kama yale yaliyotokea Tunisia kumpindua kuwa wanaota ndoto.
"