Adverts

Jan 16, 2011

SAKALA LA WALIMU KUWANGIWA CHINDI LAENDELEA KUITESA SHULE

Na Danny Tweve Mbozi.

Licha ya jitihada za serikali kwa kushirikiana na wazee wa mila wakiongozwa na chifu wa wanyamwanga kurejesha hali ya utulivu katika kijiji cha Chindi kwa kuwaopoa wale wanaotajwa kuwa vigagula, hali imeendelea kuwa tete.
Taarifa kutoka vyanzo vyetu zinaonyesha kuwa bado walimu wa shule hiyo wamepiga chenga kurejea licha ya uongozi wa wilaya kuwasihi watulize mzuka kwakuzingatia kuwa mambo yamewekwa sawa.
Walimu wamesusa kurejea kijijini hapo kwa maelezo kuwa wameathirika kisaikolojia kutokana na vitendo walivyofanyiwa vikiwemo kuingiliwa kimwili kimazingara wakiwa wamelala usiku.
Jana jioni katika pita pita yangu katika mitaa ya Vwawa wilayani hapa, mmoja wa walimu alizungumza na globu hii  ameeleza kuwa licha ya afisa elimu kuwaagiza warejee vituoni mwao juzi kabla ya kuwasikiliza, wameamua kukacha na kuendelea kupiga misele mjini Vwawa.
Mkuu wa wilaya ya Mbozi Gabriel Kimolo alitangaza kumalizika kwa matukio ya ushirikina tarehe 03 January ambapo alipongeza hatua zilizochukuliwa na wazee wa mila wakiongozwa na Chifu Chimpasya Makanda Siame kuleta mganga wa jadi ambaye aliondoa yanayodaiwa kuwa ni makombora ya kurushwa kwa mikono ya nguvu za giza mengine yakiwa yameviringishwa "chupi" zilizotambuliwa na mmoja wa walimu kuwa ni mali yake iliyotoweka katika mazingira tatanishi akiwa kwenye hadhara na tena ameivaa!!!
Tutaendelea kuwabrief maendeleo ya issue hii kupitia http://www.dtwevetz/ .blogspot.com, indaba forever