Adverts

Jan 22, 2011

shujaa wa safari lager apatikana leo

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi mil. 7 kwa Bw. Paul Luvinga alieibuka mshindi katika kinyang'anyiro cha 'Shujaa wa Safari Lager' kilichomalizika usiku huu katika ukumbi wa hoteli ya Paradise,Benjamin Mkapa Tower,Jijini Dar.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager,Fimbo Butallah na katikati ni Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,David Minja na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Mahusiano TBL,Steven Killindo.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga akimkabidhi Tuzo ya 'Shujaa wa Safari Lager' Bw. Paul Luvinga alieibuka mshindi katika kinyang'anyiro hicho usiku huu katika ukumbi wa hoteli ya Paradise,Benjamin Mkapa Tower,Jijini Dar.Katikati anaeshuhudia ni Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,David Minja.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga akitangaza mshindi wa Tuzo za 'Shujaa wa Safari Lager' usiku huu.huku Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,David Minja (katikati) na Meneja wa Bia ya Safari Lager,Fimbo Butallah wakisikiliza.
Shujaa wa Safari Lager,Bw. Paul Luvinga akionyesha Tuzo yake huku akiwa ni mwenye furaha nyingi.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA.
"