Adverts

Jan 20, 2011

(title unknown)

(title unknown): "
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Ofisi ya Bunge inapenda kuwatangazia Waheshimiwa Wabunge wote kuwa kutakuwa na mafunzo ya awali (Orientation Course) yatakayotolewa kwao kuanzia tarehe 25 Januari, 2011 mpaka tarehe 3 Februari, 2011.

Mafunzo hayo yatatanguliwa na vikao rasmi vya Vyama vya Siasa kikiwemo CCM ambacho kitakuwa na semina kuanzia tarehe 22 – 24 Januari, 2011. Kikao cha Wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kitafanyika katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam.

Kwa taarifa hii, Waheshimiwa Wabunge wanaombwa kuwasili Dar es Salaam kwa kuzingatia tarehe ya vikao hivyo vya mafunzo.

Eliakim P. M. Mrema

KAIMU KATIBU WA BUNGE

"