Adverts

Jan 14, 2011

UNA MPANGO WA KUNYWA VILEVI WEEKEND HII??ZINGATIA YAFUATAYO

UNA MPANGO WA KUNYWA VILEVI WEEKEND HII??ZINGATIA YAFUATAYO: "
1.Usinywe kilevi tumbo likiwa tupu halina chakula...kwanza utalewa haraka na inaweza kuwa mbaya kwako.
2.Usishiriki kwenye michezo ya ulevi....kuna ile michezo unakuta mnaulizana maswali mtu akishindwa kujibu adhabu yake anywe shots duuh hii mtu anaweza kunywa hata kumi mkija kushtuka ushalewa hujielewi.Kushiriki michezo ya hivi lazima ujue wapi pa kuishia kabla hujazima.
3.Jua kiwango chako...naamini kila mtu anakiwango chake cha kilevi...sio wanywaaaaaaaaaaaaaaaaaa bila kipimo.
4.Usinywe ukiwa na hasira kwani hasira inaweza kuzidi maana utajikuta unakunywa bila kipimo kisa una hasira na sio kunywa kwa kujiburudisha.
4.Usichanganye vilevi,mara umekunywa beer,whisky,brandy,wine,spirit...jamani utakuwa mtu kweli???
5.Unaweza kunywa maziwa kabla hujaanza kupata kilaji,maziwa yanasaidia kukufanya ulewe taratibu.
6.Wengi hupenda kuchanganya soda na whisky, soda na brandy au soda na spirit duuuuhhhh utalewaje haraka!!!???Hii ni mbaya japo katika hali ya kawaida wengi wanafanya.
Haya ni machache ndugu zangu,enjoy your weekend.
" indaba2010