Adverts

Jan 15, 2011

USHINDI WA TIMU YA GHANA -Oyeeee

USHINDI WA TIMU YA GHANA -Oyeeee: "

Kila Mwafrika amekuwa akifurahia majuma mawili kuwepo kombe barani; kusikia vibao vipya vya miziki ya akina Knaan na Waka Waka ya Shakira, kulisikia bara likitajwa tajwa kuliko ilivyo kawaida. Ama kweli michezo si tu starehe bali ni utamaduni, siasa na biashara….

Ila, kimpira, timu takribani zote zimetolewa. Hivyo matumaini yaliyobakia yalikuwa timu ya Waghana waliowatoa Wamarekani. Ghana ilikuwa nchi ya kwanza kupata uhuru mwaka 1957 chini ya hayati Kwame Nkrumah…yeye na Mwalimu Nyerere walikuwa waasisi wa muungano wa nchi huru za Afrika, mwaka 1963, Addis Ababa kwa Haile Sellasie.

Kampuni ya sinema ya Watanzania mjini Reading, Urban Pulse ilituletea picha hizi zinazoonyesha furaha za ushindi huo mjini humo jana Jumamosi.

" new post