Jan 16, 2011
Wajomba Wamechacha, Wamenisusia Kuku Wa Kisusio!
Wajomba Wamechacha, Wamenisusia Kuku Wa Kisusio!: "
Kwa ugali wa mtama. Leo wajomba zangu walipata habari nakuja kijijini Mzenga. Wamekasirika sijafika siku nyingi. Hasira zao wamechinja kuku na kunibanikia. Anaitwa kuku wa kisusio. Wananiambia nao wana kero zao nikawafikishie wakubwa. Wana shida ya maji na mashamba yao kuvamiwa. Nimewauliza wajomba zangu: ' Si mna mbunge wenu?' Hapo ndio nimewaudhi zaidi. Wamenitafutia na togwa ninywe! Mdharau asili yake ni mtumwa.
Hakika mchanganyiko wangu ni mgumu kwa mwingine kuelewa. Hapa nilipo sasa panaitwa Ngobedi, Mzenga, Kisarawe. Ndipo babu yangu mzaa mama alipokutana na bibi yangu Amina Binti Muhando Mwaruka. Babu yangu alikuwa Mhehe wa Iringa. Alikuja Uzaramoni kwa kazi ya ujenzi wa barabara. Bibi yangu mzaa mama anatoka katika ukoo mkubwa na maarufu. Ukoo wa Mwaruka. Ni hao akina Mbaraka Mwishehe Mwaruka. Wajomba zangu haswa."
imedowewa kwa mjengwa blog.
new post