Adverts

Jan 14, 2011

WANAUME WAKUKAA NAO MBALI

dada Dina Marios anakuja na hiii WANAUME WAKUKAA NAO MBALI: "
Wanaume wenye tabia za kitoto,hawakui hata siku moja.Hawataki kufanya kazi... kazi kulalamika na kuchukulia mambo simple tu.Kama hakui leo wakati ni mtu mzima atakua lini?yaani hawa huishia kuwa mzigo badala ye wewe kuwa mpenzi unakuwa mama yake,shangazi yake,baba yake na mpenzi at the same time.
Walalamishi,hata ufanye nini huwezi kumpendeza.Wewe ni mjinga,mwembamba sana,mnene sana,unaongea sana,una kelele sana,unacheka sana,hujapendeza...yaani wewe huna zuri.Wanachofanya ni kuua yrself estem hawa ni wabaya sana kuliko kundi lolote hapa.
Wanaume walioumizwa katika mapenzi na hawapo tayari kubadilika na kujifunza kupenda wengine.Wagumu kupenda na wameweka ukuta na ufika point huenjoy hali hiyo hivyo hata umpende vipi au kujaribu kuingia kwenye maisha yake utaishia kupoteza muda.
Wanaume wanaopenda kujipodoa kuliko wewe mwenyewe.....nyumbani mnafanya kugombania kioo lol.
Wanaume wanaopenda sana sports kuliko wewe......
mwanaume wa hivi hata uwe unamuhitaji kiasi gani kama timu yake inacheza siku hiyo utasubiri sana.Ila hawa sio wabaya sana ubaya ni siku ile ya sport anayoipenda.Ili uenjoy nafikiri itabidi ujifunze kuupenda huo mchezo.
Hivi ndivyo inavyosemekana sio usemi wangu mie nimeandika tu.Haya pia ni baadhi tu kama kuna ya ziada unaweza kuongezea.
" new post