Adverts

Jan 28, 2011

ZIARA YA KANUMBA "THE GREAT "HOLLYWOOD....3(WARNER BROTHER STUDIOS)

Nikiwa bado niko hapa Los Angeles maeneo ya Hollywood nimetembelea pia kampuni ingine ya utengenezaji wa filamu na Tv shows...ambayo ni WARNER BROS.na hapa ni mara yangu ya pili sasa nafika hapa,nimeuliza mengi na kujifunza mengi katika filamu. Hii ni moja ya vazi lililovaliwa na comedian Jeffrey Dean Morgan katika movie ya WATCHMEN(2009) iliyokuwa directed by Zack Snyder,na hili vazi lilibuniwa na Michael Wilkinson chini ya kampuni hii ya warner bros.
Hii ilitumiwa na OZYMANDIAS(MATTHEW GOODE) katika WATCHMEN(2009),NA KUWA DIRECTED BY ZACK SNYDER,VAZI KUBUNIWA NA MICHAEL WILKINSON
nikitazama logo ya kampuni hii
Hii ni mitaa ya kampuni hii iliyotengenezwa kwa ajili ya shooting wakiakisi mji wa Newyork,hivyo huwa hawaendi mbali ni humuhumu tu.
Sound stage 24 ambayo ndani ni location za shooting kama sebule ,jiko,chumba nk,taa,mic na camera zimefungwa kabisa kwa ajili ya kazi.
Harry potter,gari yake na mhusika mwenyewe,katika movie gari inaonekana inapaa lakini wapi ilikuwa hapo hapo tu,hayo mambo ya special effect.
pikipiki ya ajabu na hiyo ndege vilitumiwa na director STEVEN SPIELBERG katika HOVERCOPTER
Kupitia movie ya Harry Potter niliuliza maswali mengi kitu kilichopelekea msimamizi wangu kunionesha kwa vitendo jinsi kile kifimbo kilivyokuwa kinabadilishwa hakika nilipata elimu sawia ambayo nisingeipata pengine zaidi ya hapa.
Akinipatia maelekezo kwa uyakinifu zaidi.
Ndani ya zile SOUND STAGE kwa ndani kuko hivi,
Taa zimefungwa kwa juu na mic ambapo unaweza kushoot wakati kule nje watu hawasikii wala ninyi ndani hamsikii kelele yoyote.
Ikanibidi nipate picha kidogo
Baadhi ya tuzo ambazo kampuni hii imeshanyakua NDANI YA HOLLYWOOD
Nikielekea katika kitengo kingine kujionea ujuzi wa watu hawa.
Mojawapo ya maswali niliyouliza ni:Katika scene za kukiss na romance huwa wanafanya kweli? jibu lake huwa wanafanya kweli isipokuwa scene za kitandani hutegemea director anataka nini,mfano kama anataka waonekane wanafanya mapenzi sana basi kuna angle ambazo huweka camera na kuwaamuru wahusika kuact kama wanafanya tendo ili katika TV ionekane ni kweli..JE ni kweli HOLLYWOOD wanatoa filamu moja kwa mwaka au msanii mmoja kuigiza filamu moja kwa mwaka?..JIBU ni UONGO,kuna makampuni kadha wa kadha kama universal studio,warner bros,disneyland,columbia nk yote yanatengeneza film sasa itawezekanaje hollywood itoe filamu moja?kuhusu msanii kucheza filamu moja au zaidi inategemea na mikata aliyonayo ya kazi kwa mwaka na ratiba yake kwa kila kazi mfano mwanadada GEMA ARTETON kwa mwaka jana kuna filamu zaidi ya 3 kacheza na zote nzuri ikiwemo THE PRINCE OF PERSIA.ila haimzuii kucheza idadi ya anavyoweza.Maswali mengine nitawaandikia wakati mwingine..
"