














BAADHI YA MASWALI NILIYOULIZA WARNER BROTHER STUDIO&UNIVERSAL STUDIOS:-1.Je hollywood mnachukua mda gani kushoot filamu,JIBU:-miezi 2 mpaka 3.,,editing nayo inategemea na aina ya movie zipo zinazochukua miezi 2,na zingine 6,maana kuna vitu vingi vya kuangalia ikiwemo special effect,sound,nk.
2.Je mnapataje waigizaji hasa wapya?JIBU:-Tuna tangaza na watu wanakuja katika interview lakini pia kuna makampuni yanayohusika na casting wakati mwingine tunawapa hali halisi ya watu tunaowaitaji alafu wao hutafuta na kutuletea.
3.Mtu kama anataka kucheza movie hollywood kampuni yoyote afanyaje?JIBU:-Akisikia matangazo afanye hima kujaribu bahati yake au pia anaweza kujisajili katika hizo kampuni za casting,au anaweza kututumia Head shot(picha zake full na ya karibu) na CV na mawasiliano yake.
4.Mbona mimi mwaka 2007 niliacha hapa headshot,cv na mawasiliano yangu lakini sijawai itwa?JIBU:-Kila mtu ana bahati yake na wanaotuma hivyo vitu ni wengi kulingana na idadi inayoitajika pia sio lazima ukituma hivyo lazima uchukuliwe wewe,yoyote anawezachukuliwa kulingana na director anataka nini,lakini pia sio wote hupitia njia hizi,hollywood kila mtu kaingia kwa njia yake..tizama mtoto wa will smith katika ile movie ya Karate Kid kapata connection kupitia baba yake,kuwa na connection nalo ni muhimu,Samuel Jackson kasota sana kabla ya kuwa hapo alipo ameigiza sana katika stage lakini sasa ni star wa dunia.
5.Movie ikishakamilika inapitia hatua zipi mpaka kuwa katika DVD?JIBU:-Hupelekwa sinema huko ndiko pesa nyingi hutengenezwa,hukaa huko miezi 2 na zaidi kama movie imetokea kupendwa dunia nzima,baada ya hapo hupelekwa katika tv kuoneshwa ambapo hapo station husika hulipia kuonesha movie hiyo hapo napo pesa ingine hutengenezwa,mwisho kabisa ndio huwekwa katika DVD kuuzwa,dvd huwa hatua ya mwisho japo pia PIRATES nao wanaharibu soko maana unaweza kuta movie bado iko theatre lakini nchi fulani zina dvd zake.
NIMECHOTA KUTOKA KWENYE GLOBU YAKE KANUMBA!!